Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.
Jumla ya Wakulima 2,252 wamenufaika na mikopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ambapo jumla ya shilingi Bilioni 7.46 zimetolewa hadi kufikia Juni, 2017.
Hayo yameelezwa leo Bungeni, Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Ole Nasha alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Manase Njeza juu ya mikopo iliyotolewa na Benki hiyo mpaka sasa.
“Mpaka sasa TADB imetoa mikopo katika mikoa ya Tanga, Morogoro na Iringa, aidha wakulima wanaonufaka na mikopo...
Read More