Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Picha za Waziri Mkuu Akizundua Miongozo ya Mafunzo katika Maeneoya Kazi
Sep 16, 2017
Na Msemaji Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bibi Mary Kawar kitabu baada ya kuzindua Miongozo ya Mafunzo Katika Maeneo ya Kazi leo mjini Dodoma. Watatu kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na wapili kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na  Uwekezaji, Charles Mwijage. Kulia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Mhandisi Stella Manyanya na kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde.

Baadhi ya washiriki wa uzinduzi  wa Miongozo ya Mafunzo Katika Maeneo ya Kazi uliofanywa na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba 16, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioshiriki katika  Uzinduzi wa  Miongozo ya mafunzo Katika Maenneo ya Kazi alioufanya  kwenye ukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba 16, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama baada ya kuzindua Miongozo ya Mafunzo Mahala pa Kazi kwenye ukumbi wa LAPF  mjini Dodoma Septemba 16, 2017. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana na Ajira, Anthony Mavunde. Watatu kulia ni Mkuu wa Wlaya ya Kongwa, Deogratius, Ndejembi.

(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi