Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amezindua Kanisa, nyumba ya Mapadre na Groto katika Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Ikulu Chamwino iliyopo Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
Katika uzinduzi huo, Mhe. Rais Magufuli ameambatana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya ambaye amelibariki Kanisa, Groto na nyumba ya Mapadre na baadaye kuongoza Misa Takatifu ya Dominika ya 21 ya Mwaka “A” ndani ya Kanisa hilo.
Ujenzi wa Kanisa la Bikira Maria Imakulata, Ikulu Chamwino, Groto...
Read More