Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Akagua Magari Yaliyotaifishwa, Aagiza Yagawanywe Serikalini
Aug 25, 2020
Na Msemaji Mkuu

Sehemu ya magari 130 yaliyotaifishwa baada ya kuhusika katika matukio mbalimbali  ya uhujumu yakiwa
yamehifadhiwa katika  kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma
yaliyokaguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli leo Jumanne Agosti 25,  2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Agosti, 2020 amekagua magari yaliyotaifishwa baada ya kuhusika katika matukio ya uhujumu uchumi, na kisha kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani Jijini Dodoma.

Idadi ya magari hayo ni 130 yakiwemo makubwa na madogo yalikamatwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini, kisha wahusika kufikishwa Mahakamani na Mahakama kutoa uamuzi wa kuyataifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John

Pombe Magufuli akikagua magari 130 yaliyotaifishwa

baada ya kuhusika katika matukio mbalimbali ya uhujumu yaliyohifadhiwa

kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma leo Jumanne Agosti 25,  2020

Akizungumza baada ya kuyakagua, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Jeshi la Polisi na wote waliohusika kuwakamata waliokuwa wanajihusisha na vitendo hivyo (ikiwemo biashara haramu ya meno ya tembo) na ameagiza magari hayo yagawanywe katika taasisi mbalimbali za Serikali ili yatumike kuendesha shughuli za kuwahudumia wananchi na kuzalisha mali.

Mhe. Rais Magufuli pia amewapongeza wananchi waliojitokeza kutoa taarifa zilizosaidia kukamatwa kwa watu waliokuwa wanafanya uhalifu kwa kutumia magari hayo na amewaomba waendelee kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kukomesha vitendo hivyo.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chamwino

25 Agosti, 2020

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi