Serikali imedhamiria kuyafanya makazi ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yaliyoko Kijiji cha Mwitongo, wilayani Butiama mkoani Mara kuwa kituo cha utalii. Hayo yalisemwa jana (Jumanne, Februari 27, 2024) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa Kitongoji cha Muhumba, wilayani Butiama, akiwa njiani kuelekea Mugumu, Serengeti ambako anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Mara. Waziri Mkuu Majaliwa alimwagiza Mkuu wa Wilaya hiyo, Moses Kaegele atembelee eneo, akague na kuangalia mapung...
Read More