Waratibu wa Mradi wa Mageuzi ya Kiuchumi kwa Elimu ya Juu (HEET) kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson wameshiriki kikao cha Kikanuni kwa lengo la kujadili utekelezaji wa mradi.
Kikao hicho cha siku tatu kimefunguliwa tarehe 27 Februari, 2024 jijini Dar-es-Salaam na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Peter Msoffe ambapo alizisisitiza Taasisi zinazotekeleza mradi huo kutumia wataalamu kutoka wizarani ili kufanikisha utekelezaji wa mradi kwa kuzingatia taratibu za Benki ya Dunia.
Katika kikao hicho, Naibu Makamu Mkuu wa Taasisi Mipango Fedha na Utawala na Mratibu wa Mradi, Profesa Suzana Augustino ameeleza kuwa, mpaka sasa taasisi imeshatekeleza mradi kwa asilimia 30 kwa kuzingatia maeneo muhimu ya mradi katika taasisi ikiwepo kuhuisha vifaa vya maabara, kusomesha na kujenga uwezo kwa wafanyakazi pamoja na kuuhisha mitaala.
Profesa Suzana ametoa wito kwa taasisi zinazotekeleza mradi huo kutumia fedha walizopangiwa kwa usahihi ili kufikia malengo ya mradi kwa maendeleo ya elimu ya juu na taifa kwa ujumla.
Taarifa ya utekelezaji wa mradi wa HEET katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliwasilishwa na Mratibu Msaidizi wa mradi, Bw. Daniel Fisso.