Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akiongoza kikao wakati wa Mkutano wa 18 wa Maspika na Viongozi wa Bunge wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CSPOC) uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Yaounde Jijini Yaounde nchini Cameroon. Kikao hicho kinajadili athari za mabadiliko ya tabianchi duniani, kimefanyika leo tarehe 19 Julai, 2023. Katika mkutano huo, Mhe. Dkt. Tulia ameambatana na Mbunge wa Singida Magharibi, Mhe. Elibariki Kingu pamoja na Katibu wa Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi.
Read More