Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

RAS Geita, Viongozi wa Dini Wapongeza Ukusanyaji Maoni Maandalizi Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
Jul 19, 2023
RAS Geita, Viongozi wa Dini Wapongeza Ukusanyaji Maoni Maandalizi Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Prof. Godius Kahyarara akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Semina ya Uelimishaji Umma kuhusu Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 mara baada ya ufunguzi wa semina hiyo iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Geita Jumatano Julai 19, 2023 kwa ajili ya kukusanya maoni na kujenga uelewa kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
Na Ahmed Sagaff - Geita

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Prof. Godius Kahyarara pamoja na viongozi wa dini mkoani humo wameipongeza Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji kwa kukusanya maoni ya wadau wa maendeleo nchini kwa ajili ya kuandaa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Akizungumza na vyombo vya habari katika mahojiano maalum leo mkoani Geita, Prof. Kahyarara amesema kitendo hicho kitawasaidia wananchi kutoa maoni yao kabla ya miradi ya maendeleo tofauti na hivi sasa ambapo wananchi hutoa maoni baada ya kusikia utiaji saini wa mikataba wa miradi ya maendeleo kati ya Serikali na wawekezaji.

Amesema bado Watanzania hawafahamu maana halisi ya ubinafsishaji ndio maana kukatokea hali ya wananchi kuwa na mtazamo hasi kuhusu ubinafsishaji wa bandari.

Naye, Mwakilishi wa Umoja wa Makanisa (CCT) mkoani Geita,  Askofu Reuben Ng'wala ameeleza kwamba kitendo kilichofanywa na Ofisi ya Rais cha kukusanya maoni ya wadau wote kinaonesha namna Serikali ilivyokusudia kuwashirikisha wananchi katika kupanga maendeleo ya nchi yao.

Kwa upande wake, Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Ndg. Alhadi Kabaju amesema kitendo cha Serikali kuwashirikisha wananchi katika mipango ya maendeleo ni kitendo cha kupongezwa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi