Na Jonas Kamaleki-MAELEZO, Dodoma
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Andrew Massawe kusimamia ipasavyo mifuko mipya ya hifadhi ya jamii ili kuhakikisha michango ya watumishi inakusanywa.
Waziri Mhagama ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa kikao cha kumpokea Katibu Mkuu huyo aliyeteuliwa hivi karibuni.
“Katibu Mkuu nakuagiza uhakikishe michango inakusanywa na malipo yanalipwa kwa wakati ili kuondoa changamoto kwa wanufai...
Read More