Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mawaziri Wakutana Kujadili Maendeleo Utekelezaji wa Mradi wa Kufua Umeme Mto Rufiji
Aug 01, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_34019" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Nishati, Dkt. Merdard Kalemani akizungumza katika kikao cha Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali zinazoshiriki katika utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa Unzalishaji umeme wa maji wa Rufiji Hydropower Project leo mkoani Morogoro. Kutoka kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maeendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Ujenzi, Mhandisi Josaeph Nyamhanga akimwakilisha Waziri wa Wizara hiyo.[/caption] [caption id="attachment_34020" align="aligncenter" width="1000"] Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utali akiwakaribisha baadhi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka wizara mbalimbali waliopo mkoani humu kwa ajili ya kikao cha kufanya tathmini ya hatua za utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa maji wa Rufiji Hydropower Project kilichofanyika leo mkoani humo.Kutoka kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati, Mhe. Subira Mgalu.[/caption] [caption id="attachment_34021" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhandisi Joseph Mwalongo akizungumza katika kikao cha Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali zinazoshiriki katika utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa Unzalishaji umeme wa maji wa Rufiji Hydropower Project leo mkoani Morogoro.[/caption] [caption id="attachment_34022" align="aligncenter" width="1000"] Kiongozi wa Timu ya Wataalam Watathmini ya Athari kwa Mazingira - Mradi wa Rufiji Hydropower Project, Profesa Raphael Mwalyosi akiwasilisha mada kuhusu tathmini ya athari za mazingira katika kikao cha Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali zinazoshiriki katika utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa Unzalishaji umeme wa maji wa Rufiji Hydropower Project leo mkoani Morogoro.[/caption] [caption id="attachment_34023" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiwasilisha mada kuhusu Mkakati wa Mawasiliano na Uhamasishaji wa mradi wa uzalishaji umeme wa maji wa Rufiji Hydropower Project wakati wa kikao cha Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali zinazoshiriki katika utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa huo leo mkoani Morogoro.[/caption] [caption id="attachment_34024" align="aligncenter" width="1000"] Aliyekuwa Katibu Myeka wa mwisho wa Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere, Mzee Samweli Kasori akizungumza wakati wa kikao cha baadhi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali zinazoshiriki katika utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa huo leo mkoani Morogoro. Wizara hizo ni pamoja na Nishai, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira na Wizara ya Maliasili na Utalii.Kulia ni Mhandisi Bulton Kihaka aliyeshiriki katika kusanifu Project hiyo enzi za Hayati Baba wa Taifa.[/caption] [caption id="attachment_34025" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu walioshiriki katika kikao cha kujadili kuhusu utekelezaji wa mradi wa uzalishaji wa umeme wa maji wa Rufiji Hydropower Project wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika kikao hicho leo Mkoani Morogoro.(Picha na: MAELEZO).[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi