Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwataarifu waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kuwa imeongeza muda wa kutuma maombi kwa njia ya mtandao kwa wiki mbili kuanzia Julai 15, 2018.
Hivyo basi, tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi kupitia mtandao wa HESLB (https://olas.heslb.go.tz ) itakuwa Jumanne, Julai 31, 2018.
Aidha, tarehe ya mwisho ya kutuma nakala ngumu kwa ‘EMS’ kupitia Shirika la Posta Tanzania (TPC) ni Jumanne, Agosti 14, 2018 ili kutoa nafasi kwa HESLB kuchambua, kuhakiki na kupanga mikopo kwa...
Read More