Sehemu ya waombolezaji waliofika kushiriki katika mazishi ya marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji wakifuatilia ibada ya mazishi yaliyofanyika jana kijijini kwao Mwiruruma, Bunda mkoani Mara.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa akitoa salamu za pole kwa niaba ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa familia ya marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini kwao Mwiruruma Wilayani Bunda, mkoani Mara mapema jana.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Bi. Emma Lyimo akitoa pole kwa familia ya marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara hiyo wakati wa Ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini kwao Mwiruruma Wilayani Bunda, mkoani Mara mapema jana.
Mwakilishi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bi. Gaudensia Simwanza akitoa salamu za pole kwa familia ya marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji wakati wa Ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini kwao Mwiruruma Wilayani Bunda, mkoani Mara mapema jana.
Waombolezaji wakielekea katika viwanja vya makaburi ya familia ya marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji mara baada ya ibada ya mazishi yake iliyofanyika kijijini kwao Mwiruruma Wilayani Bunda, mkoani Mara mapema jana.
Mzee wa Kanisa la Kisabato Usharika wa Mwiruruma Wilayani Bunda Mkoani Mara Bw. John Taitus akitoa mahubiri wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara ambaye alifariki hivi karibuni kwa ajali, ibada ya mazishi yake iliyofanyika kijijini kwao Mwiruruma Wilayani Bunda, mkoani Mara mapema jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TAnTRADE) Bw. Edwin Rutageruka akitoa pole kwa Bi. Cesilia Sagati ambaye ni mjane wa marehemu Shadrack Sagati wakati wa kuaga mwili wa marehemu kabla ya kuzikwa kijijini kwao Mwiruruma Wilayani Bunda mapema jana.
Mjane wa marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji (Katikati) Bi. Cesilia Sagati akiwa kwenye ibada ya kuaga mwili wa marememu mume wake Kijijini kwao Mwiruruma Wilayani Bunda, mkoani Mara kabla ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya familia Kijijini hapo.
Wawakilishi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO)wakiongozwa na Bi. Gaudensia Simwanza (kushoto) wakiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji ambaye alifariki hivi karibuni kwa ajali, ibada ya mazishi iliyofanyika kikijini kwao Mwiruruma Wilayani Bunda mapema jana.
Mjane wa marehemu marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji (Katikati) Bi. Cesilia Sagati akiweka shada la maua kwenye kaburi wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini Mwiruruma, Wilayani Bunda mkoani Mara jana.
Mwili wa marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji ukiwekwa kaburini mara baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kijiji cha Mwiruruma Wilayani Bunda Mkoani Mara jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TAnTRADE) Bw. Edwin Rutageruka akitoa salamu za pole kwa familia ya marehemu Shadrack Sagati wakati mazishi yaliyofanyika Kijijini kwao Mwiruruma, Bunda mkoani Mara jana.
Sehemu ya waombolezaji wakishindwa kuzuia hisia zao wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji kabla ya kuzikwa kijijini kwao Mwiruruma, Bunda mkoani Mara.
Sehemu ya Wanatasnia ya Habari na Mawasiliano wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjane wa maremu Shadrack Sagati Bi. Cesilia Sagati (watano kutoka kulia) mara baada ya mazishi yaliyofanyika jana Kijijini kwao Mwiruruma, Bunda mkoani Mara.
Waombolezaji pamoja na ndugu jamaa na marafiki wakijiandaa kuweka mwili wa marehemu Shadrack Sagati kaburini mara baada ya ibada ya mazishi yaliyofanyika jana kijijini kwao Mwiruruma, Bunda mkoani Mara.
(Picha na Frank Mvungi- MAELEZO, Mara)