Na Jacquiline Mrisho
Katika Mwaka wa Fedha 2018/19, uzalishaji wa zao la pamba umefikia tani 221,600 ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 67 kutoka tani 133,000 zilizozalishwa mwaka 2017/18.
Takwimu hizo zimetolewa leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Omary Mgumba alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Igunga, Dkt. Dalaly Kafumu lililohoji ni lini Serikali itashughulikia changamoto za wakulima hasa kwa kupewa mbegu bure.
Mhe. Mgumba amesema kuwa mojawapo ya changamoto za wakulima wa pamba katika kuongeza tija...
Read More