Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Mji wa Serikali chenye hadhi ya daraja A, Mtumba Jijini Dodoma, Desemba 2, 2021. Uzinduzi wa kituo hicho ni miongoni mwa matukio ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, wa pili kushoto, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro, Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Muonekano wa Sehemu ya jengo la kitega uchumi unaotekelezwa na jiji la Dodoma katika mji wa Serikali Mtumba, ambalo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amelitembelea Jijini Dodoma Desemba 2, 2021. Mradi huo unajengwa kwa awamu mbili na utagharimu shilingi bilioni 59.3, Jengo hilo lina Hotel, maduka na huduma za kibenki, kumbi za mikutano ikiwemo mkubwa wenye uwezo wa kuhudumia washiriki 1000 kwa wakati mmoja na kumbi ndogo 6 zenye uwezo wa kuhudumia 120 kwa wakati mmoja.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa jengo la kitega uchumi unaotekelezwa na jiji la Dodoma katika mji wa Serikali Mtumba, ambalo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amelitembelea Desemba 2, 2021. Ukaguzi huo ni miongoni mwa matukio ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania.
Muonekano wa Sehemu ya jengo la kitega uchumi unaotekelezwa na jiji la Dodoma katika mji wa Serikali Mtumba ambalo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amelitembelea Jijini Dodoma Desemba 2, 2021. Mradi huo unajengwa kwa awamu mbili na utagharimu shilingi bilioni 59.3, Jengo hilo lina Hotel, maduka na huduma za kibenki, kumbi za mikutano ikiwemo mkubwa wenye uwezo wa kuhudumia washiriki 1000 kwa wakati mmoja na kumbi ndogo 6 zenye uwezo wa kuhudumia 120 kwa wakati mmoja.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda mti katika eneo la Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar lililotolewa katika mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma, Desemba 2, 2021. ikiwa ni miongoni mwa matukio kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania.