Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Dkt. Mwinyi Aushukuru Mfuko wa Aga Khan Kwa Ushirikiano Zanzibar
Feb 18, 2026
Rais Dkt. Mwinyi Aushukuru Mfuko wa Aga Khan Kwa Ushirikiano Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Amekutana na Mwakilishi wa Kidiplomasia wa Mfuko wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN) Kanda ya Afrika Mashariki, Ndg. Amin Mawji, Ikulu, Zanzibar.
Na Mwandishi Wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na Mwakilishi wa Kidiplomasia wa Mfuko wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN) Kanda ya Afrika Mashariki, Ndg. Amin Mawji, aliyefika Ikulu, Zanzibar, leo tarehe 18 Februari 2026, akiambatana na Ndg.Rahim Bhaloo, Mratibu wa AKDN Zanzibar.

Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mfuko huo, hususan katika maeneo ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dkt. Mwinyi ameushukuru Mfuko wa Maendeleo wa Aga Khan kwa mchango wake mkubwa kwa Zanzibar, ikiwemo utoaji wa huduma za afya, programu za mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji katika sekta mbalimbali, pamoja na uwekezaji na misaada katika sekta ya elimu.

Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano huo kwa manufaa ya wananchi wa Zanzibar, akieleza kuwa juhudi za pamoja kati ya Serikali na wadau wa maendeleo zina mchango mkubwa katika kuharakisha ustawi wa kijamii na kukuza uchumi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi