[caption id="attachment_25012" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu taarifa iliyotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) ambapo alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya Shirika hilo uchumi wa nchi uko imara ukilinganisha na nchi zilizofanyiwa tathimini.[/caption]
Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Serikali kupitia Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan imesema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) uchumi wa nchi uko imara ukilinganisha na nchi zilizofanyiwa tathimini.
Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akiongea na vyombo vya habari juu ya maoni ya wataalam wa uchumi kutoka IMF ambao wamemaliza ziara yao hapa nchini Desemba 12, 2017.
"Ripoti ya IMF inaonesha katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017 uchumi umekua kwa asilimia 6.8 takwimu ambazo ni za juu katika chumi zinazokua kwa kasi na ikizidi nchi kadhaa zilizofanyiwa tathmini mwaka 2017 zikiwemo za Ulaya," amefafanua Dkt. Abba.
Ameendelea kusema, mapato ya nchi yameongezeka kutoka Shilingi Trilioni 9.9 mwaka 2015 kufikia Shilingi Trilioni 14 mwaka 2017.
[caption id="attachment_25013" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)kuhusu taarifa iliyotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) ambapo alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya Shirika hilo uchumi wa nchi uko imara ukilinganisha na nchi zilizofanyiwa tathimini.[/caption]Aidha, kutokana na usambazaji mzuri wa chakula mfumuko wa bei ya chakula ulishuka hadi kufikia asilimia 4.4 ikiwa ni chini ya lengo ambalo IMF ilitabiri mfumuko ungekuwa asilimia 5.
Aidha amesema, Serikali imeendelea kulipa madeni ya ndani ambapo mpaka sasa Shilingi bilioni 900 zimeshalipwa na shilingi bilioni 37 zimelipa madeni ya watumishi wa Serikali.
Vile vile Serikali imefanikiwa kufufua viwanda vipya 17 kupitia ofisi ya Msajili wa Hazina ambavyo vilikuwa vimekufa na viwanda vingine vipya zaidi ya 500 vimeanzishwa ambavyo na kuhesabika kuwa kigezo kipya cha uchumi kutokana na kutoa ajira kwa watanzania pamoja na kulipa kodi kwa Serikali.
Msemaji wa Serikali ameeleza kuwa kwa kawaida uchumi wa nchi hausimami na kwamba kuna shughuli nyingine mpya zinaingia katika uchumi na kutumika kama kigezo cha kukua kwa uchumi.
Timu hiyo ya wataalamu kutoka IMF iliongozwa na Bw. Mauricio Villafuerte ambapo walifanya ziara juu ya tathimini ya uchumi katika nchi Saba Afrika ikiwemo Tanzania pamoja na Msumbiji, Rwanda, Nigeria, Uganda, Senegari na Cape Verde.