[caption id="" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka kwa tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa unaofanyika katika ukumbi wa Hazina leo Mkoani Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_20936" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI Mhe.Tixon Nzunda akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka kwa tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa unaofanyika katika ukumbi wa Hazina leo Mkoani Dodoma.[/caption]
(PICHA NA DAUDI MANONGI)
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amesema umefika wakati ambapo nchi nyingine zije Tanzania kujifunza mambo ambayo tumefanikiwa ikiwa ni pamoja na masuala ya madini, usafiri wa Umma kupitia mabasi ya mwendokasi na masuala ya ugatuaji wa madaraka.
Mhe. Jafo ameyasema hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa akifungua Warsha ya Kitaifa Juu ya Maboresho ya Huduma za Umma na Ugatuaji wa Madaraka Kwenye Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri, Manispaa na Majiji pamoja na Wakurugenzi kutoka TAMISEMI.
[caption id="attachment_20939" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo(KULIA) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongela wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa na Taasisi ya Uongozi Institute wanaoendesha warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka kwa tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inayofanyika katika ukumbi wa Hazina leo Mkoani Dodoma.[/caption]“Mara nyingi tumekuwa tukienda nchi kama vile Japan kujifunza katika maeneo mbalimbali ambayo wamefanikiwa kama vile masuala ya uchumi, Lakini pia Tanzania tumeanza kupokea mataifa mbalimbali ambayo yanakuja kujifunza mambo ya usafiri wa Umma kupitia mradi wa mabasi ya mwendokasi ambao umekuwa ni kivutio kikubwa kwa nchi nyingi za Afrika,” amesema Jafo.
Ameendelea kwa kusema, mambo ya kuja kujifunza hapa nchini kwa mataifa mengine yanaendelea kuongezeka hasa katika kipindi hichi cha Serikali ya Awamu ya Tano ambapo Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameleta mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya madini ambayo sasa itainufaisha nchi na wananchi wanyonge tofauti na ilivyokuwa awali.
Jafo amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano inatia mkazo suala la ugatuaji wa madaraka ili kuendelea kuwawezesha wananchi kuwa na sauti katika maeneo yao ikiwemo kuchangia maendeleo ya nchi kupitia viongozi wao.
[caption id="attachment_20941" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI Dk Zainabu Chaula(kushoto mwenye miwani) pamoja na washiriki wengine wa warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka kwa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(hayupo pichani) leo mkoani Dodoma.[/caption]Aidha Mhe. Jafo amesema kuwa utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano umeasisiwa na wananchi wenyewe ambao Rais Magufuli anafanya kazi kutokana na ajenda za wananchi ya kutaka mabadiliko kupitia uchumi wa viwanda ifikapo 2025.
Hata hivyo, Jafo amewataka watumishi wa Umma kubadilika na kufikia malengo ambayo wamewekewa katika kutimiza shughuli zao za kila siku.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza ambaye pia ni mshiriki wa warsha hiyo amemuahidi Mhe. Jafo kujadili kwa mapana tathimini juu ya masuala ya ugatuaji wa madaraka ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.