Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wizara ya Maliasili na Utalii na Kasi ya Kudhibiti Migongano
Mar 03, 2026
Wizara ya Maliasili na Utalii na Kasi ya Kudhibiti Migongano
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Kijaji, katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanyamapori Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Viwanja vya Nanenane, Njiro, jijini Arusha.
Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameitaka  Taasisi ya  Utafiti wa Wanyamapori  Tanzania (TAWIRI) kukamilisha zoezi la kuwafunga tembo viongozi wa  makundi  mikanda ya visukuma mawimbi (GPS COLLARS) ili kufuatilia mienendo yao na kudhibiti Migongano kati yao na binadamu.

Dkt. Kijaji amesema hayo  leo 03 Machi, 2026 katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanyamapori Duniani ambayo  Kitaifa yamefanyika  Viwanja vya Nanenane vilivyopo Njiro jijini Arusha.

Aidha, amesema kuimarika kwa Uhifadhi wa rasilimali za wanyamapori kumechochea  ukuaji wa sekta ya utalii nchini. “ idadi ya watalii imeongezeka kutoka 5,360,247 mwaka 2024 hadi watalii 5,935,561 mwaka 2025 sawa na ongezeko la asilimia 10.73” amefafanua Dkt. Kijaji

Dkt. Kijaji amesema Serikali inaendelea na  mikakati  ya kuhakikisha wanyamapori wanakuwa salama na watu wanakuwa salama  “Wanyamapori ni rasilimali muhimu katika uchumi wa nchi ambapo  kupitia utalii kumekuwa na ongezeko la fedha za kigeni kutoka Dola za Marekani Bilioni 3.9 hadi kufikia dola bilioni 4.4 sawa na ongezeko la asilimia 12.82.”

Akibainisha  changamoto za sekta ya uhifadhi, amesema Kuongezeka kwa migongano baina ya binadamu na wanyamapori wakali na waharibifu kunasababisha  mahusiano hasi kati ya binadamu na wanyamapori “ nielekeze kufanyika tafiti za kimkakati ili kubaini mbinu mpya za kukabiliana na changamoto hii” amehimiza Dkt.Kijaji

Aidha, amesema  udhibiti wa migongano unaendelea ambapo  tembo 176 viongozi wa makundi wamefungwa mikanda   Ya visukuma mawimbi ili kufuatilia mienendo yao na kuthibiti uharibifu. Pia Kwa mamba na viboko tayari vizimba 18 vimejengwa  maeneo mbalimbali nchini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi