Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TBS Kuendelea Kulinda Soko la Tanzania
Jan 13, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_50129" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania Dkt.Athuman Yussuf Ngenya akipewa maelezo juu ya bidhaa zilizozalishwa na wajasiriamali waliopata alama ya ubora katika hafla ya utoaji vyeti iliyofanyika makao makuu ya TBS Ubungo mwishoni kwa wiki TBS ilitoa jumla ya leseni 96 kati ya hizo leseni 27 ni wajasiriamali wadogo na leseni 1 ni ya mfumo. Leseni hizi ni majumuisho kwa kipindi cha mwezi oktoba mpaka Disemba mwaka 2019[/caption]

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA LA Viwango Tanzania (TBS), limesema hakuna bidhaa ya chakula au vipodozi itakayoruhusiwa kuingia kwenye soko la Tanzania kama haijasajiliwa au kuthibitishwa ubora wake na shirika hilo.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Saalam na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt Athuman Ngenya, kwenye hafla ya utoaji wa leseni na vyeti vya ubora 96 kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini ambao wamekithi viwango vya ubora

Alisisitiza kwamba ni lazima majengo ya kuzalisha, kuhifadhi au kuuzia chakula, vipodozi pamoja na vyombo vinavyobeba bidhaa hizo ikiwemo magari ya kubebea nyama yawe yamesajiliwa na Shirika hilo, ndipo yataruhusiwa kutumika. Alisema majukumu ya shirika hilo ni pamoja na usajili wa vyakula, vipodozi na majengo kwa mujibu wa marekebisho ya Sheria ya Viwango na mabadiliko Sheria ya Fedha Namba 8 ya mwaka 2019.

Kwa upande wa vyeti na leseni zilizotolewa, Dkt. Ngenya alisema zimetolewa kwa wazalishaji wa bidhaa wakubwa, wa kati na wadogo baada ya mifumo inayotumika kuzalishia bidhaa zao kuthibitishwa na kukidhi matakwa ya viwango kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba, mwaka jana.

Alisema zimetolewa leseni na vyeti 96,vyeti 27 kwa wajasiriamali wadogo na kimoja ni kutokana na ubora wa mifumo. Dkt.Ngenya aliwataka wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini kuhakikisha wanazalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango vya ubora kwa mustakabali ya kulinda afya za watumiaji wa bidhaa hizo ndani na nje ya nchi.

Alisema leseni na vyeti hivyo vilivyotolewa kwa wazalishaji hao, vitazisaidia bidhaa zao kuongeza imani kwa umma juu ya ubora wa bidhaa wanazozizalisha, kukubalika sokoni na kupata faida ya kushindana na kuingia katika soko la Afrika mashariki pasipo kufanyiwa vipimo zaidi.

"Natoa na pongezi kwa Wazalishaji aliofanikiwa kupata vyeti na leseni za ubora muwe mabalozi wazuri kwa kuzingatia matumizi ya viwango ili kuweza kutimiza malengo ya ujenzi wa Tanzania ya viwanda," alisema na kuongeza;

"Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli inaendelea kuwahudumia wajasiriamali kwa kupata huduma za TBS bila malipo ya gharama za ukaguzi na upimaji."

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi