Rais Mwinyi Akagua Miradi ya Maendeleo Mjini Magharibi
Jul 08, 2021
Na
Jacquiline Mrisho
Mwananchi wa Shehia ya Welezo Bw. Ameir Ismail Hassan alipopkuwa akielezea changamoto ya kutopatikana kwa huduma ya Maji Safi na Salama katika Shehia hiyo leo wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati alipotembelea Vyanzo vya Maji Safi na Salama vya Welezo akiwa katika ziara ya Mkoa wa Mjini Magharibi iliyoanza leo kwa kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo.[Picha na Ikulu - Zanzibar.]
Mwananchi Khamis Ali Haji akieleza malalamiko mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) yanayohusiana na mgogoro wa ardhi wakati alipotembelea Vyanzo vya Maji Safi na Salama vya Welezo akiwa katika ziara ya Mkoa wa Mjini Magharibi iliyoanza leo kwa kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo.[Picha na Ikulu - Zanzibar.]
Viongozi mbali mbali wakisikiliza taarifa ya utekelezaji ya Mkoa wa Mjini Magharibi Iliyowasilishwa mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi kabla ya ziara ya kutembelea miradi ya Maendeleo katika Mkoa huo leo.[Picha na Ikulu - Zanzibar]