Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mitambo Mipya ya TBC Kuwekwa Eneo la Gitsmii Kuimarisha Usikivu Manyara.
Jan 24, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_50380" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Manyara katika mkutano wa Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Alexandar Mnyeti uliokuwa na lengo la kuboresha Sekta ya elimu mkoani hapo wakati Waziri alipokua kwenye ziara ya kukagua mitambo ya usikivu ya TBC iliyopo Mkoani hapo eneo la Gitsimii pamoja na kuzungumza na wadau wa tasnia ya habari Januari 23, 2020.[/caption]

Na Shamimu Nyaki –WHUSM, Manyara.

Serikali imeanza kuhamisha mitambo ya Usikivu ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutoka katika jengo la Mkoa wa Manyara kupeleka katika eneo la Gitsmii ambalo lina  mwinuko utakaosaidia kuimarisha usikivu katika mkoa huo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo alipofanya ziara katika mkoa huo jana Januari 23,2020 ya kukagua mitambo hiyo ambayo imekua na changamoto ya kutosikika vizuri katika maeneo mengi ndani ya mkoa huo.

“Tunafahamu changamoto ya usikivu wa TBC hapa Manyara ndio maana nimekuja pamoja na wataalam kuona namna ya kutatua changamoto hiyo na tayari tumeshaanza mpango wa kuhamisha mitambo kupeleka eneo waliloshauri wataalam wetu kwamba litaimarisha usikivu katika mkoa huu”alisema Dkt.Mwakyembe.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dkt.Ayoub Ryoba amesema kuwa tayari ofisi imeagiza mtambo wa “Wats” 2000 ambao ndio unaotakiwa kuwekwa katika eneo hilo ili matangazo ya TBC yawafikie watu wengi wa mkoa wa manyara na maeneo jirani.

“TBC ni chombo cha umma lazima kiwafikie wananchi wote ndio maana tunaendelea kuimarisha usikivu katika maeneo mbalimbali na mpaka sasa tumeshafikia asilimia zaidi ya 70”alisema Dkt Ryoba.

[caption id="attachment_50381" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Alexandar Mnyeti akizungumza na viongozi wa Mkoa huo katika kikao cha kujadili maendeleo ya elimu na namna ya kuboresha ufaulu wa wanafunzi wa mkoa huo uliofanyika Januari 23,2020.[/caption]

Wakati huo huo.Dkt Mwakyembe ameuagiza Mkoa huo kushirikiana na TANROADS pamoja na TANESCO kutengeneza barabara inayoelekea sehemu iliyosimikwa mitambo hiyo pamoja na umeme na maji kwakua ni miundombinu muhimu inayohitajika  katika eneo hilo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Alexandar Mnyeti amesema kuwa wananchi wamekua wakilalamika kukosa matangazo ya TBC lakini Serikali imatambua hilo na imeanza kulifanyia kazi.

“Katika Sekta ya Utamaduni na Michezo Mkoa huu unafanya vizuri sana hasa katika michezo ya riadha na uhifadhi wa mila na desturi  changamoto kubwa ni usikivu wa TBC redio  ni hafifu mno tunaamini ujio huu utaleta matokeo mazuri hivi karibuni”alisema Mhe.Mnyeti.

[caption id="attachment_50382" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO Bw.Rodney Thadeus akizungumza na wadau wa tasnia ya habari wa Mkoa wa Manyara(hawapo pichani) katika kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) kilichokua na lengo la kusikiliza na kutatua changamoto wanazokutana nazo katika kutekeleza majukumu yao.[/caption]

Katika hatua nyingine Waziri Mwakyembe amewasisitiza waandishi wa habari wa mkoa huo kufanya kazi yao kwa weledi na uadilifu kuzingatia Sheria ya Huduma za Habari na Sheria ya upatikanaji wa habari,ambapo amewasisitiza kuwa mwisho wa uandishi wa mtaani ni Desema 2021.

Mhe.Waziri ameongeza kuwa kazi ya uandishi wa habari ni taaluma kama taaluma nyingine hivyo wanapaswa kuhakikisha wanafuata misingi ya taaluma hiyo ikiwemo kutoa habari kwa usahihi na kwa wakati sahihi pamoja na kutumia vyanzo sahihi.

Hata hivyo Mhe.Waziri alipata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa Mkoa huo katika kikao kilichoandaliwa na Mkuu wa Mkoa Mhe.Alexandar Mnyeti kilichokua na lengo la kuimarisha sekta ya elimu pamoja na ufaulu wa wanafunzi wa mkoa huo ambapo amewataka viongozi hao kutorudi nyuma katika kuendeleza elimu kwa vijana walioko shuleni.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi