Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara: Serikali Yajivunia Juhudi na Mafanikio ya Sekta ya Utalii
Nov 30, 2021
Na Jacquiline Mrisho

Na Beatrice Sanga - MAELEZO

Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amesema Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, imekuwa ikiimarisha juhudi za utangazaji wa vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi tangu Taifa lilipopata Uhuru Mwaka 1961, na kuifanya sekta hiyo kuwa na umuhimu katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya Wananchi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Novemba 30, 2021 Jijini Dodoma, Naibu Waziri huyo amesema Serikali imeendelea kubuni na kutekeleza mikakati mbalimbali ikiwemo kutumia ofisi za Balozi za Tanzania nje ya nchi kutangaza Utalii, kuandaaa na kushiriki kwenye makongamano, maonyesho na ziara za utangazaji utalii katika masoko ya msingi kwenye nchi mbalimbali duniani.

Amezitaja nchi hizo kuwa ni Uingereza, Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Italia na Hispania, pia amesema Serikali imekuwa ikitafuta masoko mbalimbali ya kimkakati kwenye nchi kama vile china, Urusi, India, Israel, Uturuki na Falme za Kiarabu lengo likiwa ni kuimarisha matumizi ya TEHAMA, kuandaa ziara za mafunzo kwa waandishi wa habari wa Kimataifa, Mawakala wa Utalii na Mawakala wa Usafirishaji kwa ajili ya kusaidia kutangaza utalii wa  nchi yetu.

“Wizara imeendelea kutumia ofisi za Balozi  za Tanzania nje ya nchi  kimkakati  kutangaza na  kuhamasisha utalii kikanda  na Kimataifa,  kutumia mabalozi wa hiari kama ambavyo mmekuwa  mkisikia kila mara  tunatangaza  mabalozi wa hiari na  tunawaalika watanzania wote  ambao  ni wazalendo  na wenye kuipenda nchi yao  kuwa mabalozi, sio lazima  ulipwe  hata ukiwa umeamua kama mzalendo kuitangaza nchi yako sisi tuna watunuku kwa  kuwapa ubalozi wa hiari’, alisema Mhe Masanja.

Mhe. Masanja amesema katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Serikali kupitia sekta ya Maliasili na Utalii imewezesha Taifa kupata mafanikio mbalimbali ikiwemo kukua na kuimarika kwa Sekta ya Utalii   ambapo katika miaka 60 iliyopita Serikali iliimarisha utalii kwa kusimamia ipasavyo utekelezaji  wa  mikakati ya  kukuza vivutio  mbalimbali vya utalii   vikiwemo hifadhi za wanyama pori,  maporomoko ya maji, milima,  misitu  ya mazingira asilia, utamaduni, fukwe na mali kale kupitia uendelezaji wa vivutio hivyo  na kupelekea Kuongezeka kwa idadi ya watalii na mapato ambapo sekta hiyo huchangia takribani asilimia 25 ya fedha za kigeni lakini zaidi ya asilimia 17 katika pato la taifa na idadi ya watalii kutoka nchi mbalimbali imeongeeka kutoka  watalii 9847 mwaka 1960  hadi kufikia watalii 1,527,230  mwaka 2019.

Ameongeza kuwa pamoja na mafanikio hayo, Tanzania kupitia Shirika la Hifadhi la Taifa  limetangazwa kuwa mshindi wa kundi la dhahabu  miongoni mwa  wa washindi 51 wa  kutoka nchi 39  duniani wa tuzo ya huduma  za viwango  vya  kimataifa kwa mwaka 2020 pia hifadhi tano za taifa   ambazo ni Kilimanjaro  Serengeti  Mkomazi  Manyara na Arusha zimepata tuzo  bora  ya huduma za viwango  vya kimataifa  kwa mwaka 2020 lakini pia hifadhi tano za Taifa  ambazo ni Serengeti, m Mkomazi, Manyara, na Arusha  zimepata tuzo bora za huduma ya viwango  vya Kimataifa kwa mwaka 2020.

Pia, Naibu Waziri Masanja ameeleza kuwa katika kuboresha huduma katika sekta ya utalii seriali imeanzisha mfumo wa kielektroniki  ujulikanao kama “Accomodation Service in Tanzania” (ASET) ambapo mfumo huu unawezesha wamiliki wa huduma za maradhi kujitathmini kwa kutumia vigezo vya kupanga huduma za maradhi katika ubora vilivyowekwa na jumuiya ya Afrika Mashariki lakini pia Serikali itaendelea kutoa mafunzo kwa watoa huduma  za maradhi kuruhusu namna ya  kusajili wageni kwa kutumia mfumo huo.

Aidha, Mhe. Masanja ameongeza kuwa ili kudhibiti ujangili, uvunaji haramu wa mazao ya misitu na uvamizi katika maeneo yaliyohifadiwa Serikali imeendelea kuweka juhudi katka kulinda rasilimali hizi ikiwa ni pamoja na kuanzisha kikosi kazi cha taifa dhidi ya ujangili kinachojumuisha wadau wengine kuanzisha jeshi la uhifadhi wa wanyama pori na misitu na kuandaa mkakati wa kitaifa   wa kupambana na  ujangili wa wanyama pori ulioanza kutekelezwa tangu mwaka  2014

“Wananchi ni mashahidi kwamba sasa hivi sisi ni Jeshi kamili na ukisikia wananchi wanalialia sana huko  ni  kwa sababu tumeendelea kuimarisha ulinzi wa maeneo yote ya hifadhi ili kuhakikisha rasilimali hizi tulizopewa na Mwenyezi Mungu tunazilinda kwa ajili ya  kuendelea kuongeza ajira kwa wananchi lakini pia kukuza uchumi wa Taifa”, Alisema.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi