Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameshiriki ufunguzi wa mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi na Serikali Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM). Mheshimiwa Majaliwa ameshiriki mkutano huo uliofunguliwa na Rais wa Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni akimwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mkutano huo wa siku mbili umeanza leo Ijumaa, Januari 19, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Ruwenzori, Kampala nchini Uganda. Katika mkutano huo, Rais wa Uganda alikabidhiwa rasmi uenyekiti wa kundi hilo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya...
Read More