Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Halmashauri Rukwa Zaruhusiwa Kutengeneza Madawati
Jan 29, 2024
Halmashauri Rukwa Zaruhusiwa Kutengeneza Madawati
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Makongoro Nyerere akizungumza leo wakati wa Mkutano wa Waandishi wa Habari na Mkuu wa Mkoa pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri uliofanyika leo mkoani humo
Na Ahmed Sagaff – Maelezo

Wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani Rukwa wameruhusiwa kutengeneza madawati ili wanafunzi waweze kusoma bila uwepo wa changamoto ya kukosekana kwa madawati.

Akizungumza leo mjini Sumbawanga, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Makongoro Nyerere amesema shule nyingi mkoani humo zina madawati akieleza kuwa huenda shule chache ambazo hajatembelea ndizo zina uhaba wa madawati.

“Rais amewaruhusu Wakurugenzi wa Halmashauri zote kutafuta njia ya kuhakikisha shule zinapata madawati,” ameeleza Mhe. Makongoro.

Amesema watumishi wa Mkoa wa Rukwa watafanya ufuatiliaji na tathmini ili kubaini usahihi wa uvumi unaoenezwa kuwa Serikali ya Rais Samia imejenga majengo ya shule bila kuweka madawati.

Tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021 Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akiendeleza utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa shule za msingi na sekondari kwa ufanisi mkubwa huku akiwasimamisha kazi wakurugenzi wanaokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi