*Azindua Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini
*Asema utashusha bei ya vyakula mijini
CHANGAMOTO ya usafiri nchini, hususan maeneo ya vijijini kuwa historia baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzindua Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).
Amesema wakala huo utasaidia kuimarisha mtandao wa barabara za vijijini na kuwawezesha wananchi wengi kusafiri na kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi, hivyo kukuza uchumi.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 02, 2017) wakati akizindua wakala huo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango,...
Read More