Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mamlaka za Maji Ziige Mfano wa Tanga Uwasa Uhifadhi wa Vyanzo Vya Maji.
Jul 11, 2017
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_6266" align="aligncenter" width="892"] Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (TANGA UWASA) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari mapema hivi karibuni Ofisini kwake kuhusu mafanikio yatokanayo na utafiti kupitia Filamu ya Mamba wa Zigi. Filamu hiyo imeelezea namna wananchi wanaozunguka maeneo ya mto Zigi unaounganisha wilaya za Muheza, Mkinga na Tanga wanavyoathiriwa na uharibifu wa vyanzo vya maji. (Na: Mpiga Picha Wetu)[/caption]

Na: Mwandishi Wetu

 

TAARIFA ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2004 inaonesha kuwa ifikapo mwaka 2025, nchi za Bara la Afrika hususani zilizopo kusini ya jangwa la Sahara, zitakumbwa na upungufu mkubwa wa maji kutokana na ongezeko la watu na matumizi ya maji yasiyo endelevu.

 

Aidha inakadiriwa kuwa upatikanaji wa maji kwa kila mtu kwa mwaka utapungua toka mita za ujazo 2,300 za sasa hadi 1,500 ifikapo 2025 kutokana tatizo la kuharibika na kupotea kwa vyanzo vya maji.

 

Pamoja na umuhimu wa maji kueleweka na kila mwananchi, taarifa zinaonyesha kuwa vyanzo vingi vya maji nchini vimeendelea kuharibika kwa kasi na kusababisha maji kupungua katika mito na maziwa mengi.

[caption id="attachment_6267" align="aligncenter" width="1000"] Afisa Uhusiano wa Umma wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (TANGA UWASA) Bi. Dorah Killo akielezea jambo wakati wa mkutano baina ya Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Uwasa, Mhandisi Joshua Mgeyekwa (katikati) na waandishi wa habari mapema hivi karibuni Ofisini kwake kuhusu mafanikio yatokanayo na utafiti kupitia Filamu ya Mamba wa Zigi. Filamu hiyo imeelezea namna wananchi wanaozunguka maeneo ya mto Zigi unaounganisha wilaya za Muheza, Mkinga na Tanga wanavyoathiriwa na uharibifu wa vyanzo vya maji. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni iliyotengeneza Filamu hiyo Bw. Humphrey Mgema .[/caption]

Ili kukabiliana na hali hiyo, Serikali inatekeleza Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji 2006-2025 inayolenga katika kuhimiza na kusisitiza usawa na utashi katika utunzaji na usimamizi wa rasilimali za maji katika maeneo ya mijini na Vjijini.

Kwa hapa nchini, huduma ya usambazaji wa maji safi na salama na uondoaji wa majitaka Mijini inatekelezwa na Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira katika Miji Mikuu ya Mikoa, Wilaya, Miji Midogo.

Inaelezwa kuwa wastani wa uzalishaji wa maji katika miji mikuu ya mikoa imepungua kutoka lita milioni 470 kwa siku mwezi Machi 2016 hadi kufikia lita milioni 400 kwa siku mwezi Machi, 2017 kutokana na kupungua kwa wingi wa maji katika vyanzo vya maji katika maeneo mbalimbali nchini.

  [caption id="attachment_6268" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (TANGA UWASA) wakifuatilia mkutano baina ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo (hayupo pichani) na wandishi wa habari mapema hivi karibuni Ofisini kwake kuhusu mafanikio yatokanayo na utafiti kupitia Filamu ya Mamba wa Zigi. Filamu hiyo imeelezea namna wananchi wanaozunguka maeneo ya mto Zigi unaounganisha wilaya za Muheza, Mkinga na Tanga wanavyoathiriwa na uharibifu wa vyanzo vya maji.[/caption]

Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (TANGA UWASA) kwa kushrikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga mwaka 2015 ilizindua Filamu ya utafiti ya Mamba wa Zigi iliyoelezea kuhusu uharibifu wa mazingira katika milima ya usambara ambayo ndio chanzo kikuu cha upatikanaji wa maji Jijini Tanga.

Akizungumza hivi karibuni na Waandishi wa vyombo vya Habari Jijini humo, Mkurugenzi Mtendaji wa TANGA UWASA, Mhandisi Joshua Mgeyekwa anasema kabla ya uzinduzi wa filamu, mamlaka hiyo ilikuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira katika mito midogo midogo inayounganisha Mto Zigi na Bwawa la Mabayani na hivyo kutishia uendelevu wa huduma ya kusambaza maji Jijini Tanga.

Anasema utafiti wa filamu hiyo ulionyesha kuwa shughuli za kijamii na kiuchumi zikiwemo kilimo, ukataji miti, uogeshaji mifugo, na uchimbaji wa madini ulichangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira katika maeneo mengi Vijini vinavyozunguza Mto Zigi unaounganisha Wilaya za Muheza, Mkinga na Tanga.

“Kufuatia hali ya uharibifu wa vyanzo vya maji katika maeneo hayo, mwaka 2009 tuliamua kutumia fursa ya utafiti kupitia filamu kwa kuwasiliana na wadau mbalimbali wa mazingira kwa ajili ya kutoa elimu na kuendesha tafiti ili kuonyesha hatua zinazopaswa kuchuliwa katika kulinda na kuhifadhi vya maji ya Mto Zigi” anasema Mhandisi Mgeyekwa.

Kwa mujibu wa Mhandishi Mgeyekwa anasema tangu kuzinduliwa kwa filamu hiyo mafanikio mbalimbali yameweza kupatikana ikiwemo uanzishaji wa Umoja wa Wakulima Wahifadhi Mazingira Kihuhwi Zigi (UWAMAKIZI) ambapo jumla ya vijiji 8 vimejiunga katika Umoja huo ulioanzishwa mwaka 2013 kwa ajili ya ulinzi wa ardhi, maji na mazingira katika eneo la vyanzo vya Mto Zigi.

Umoja huu ulianzishwa mwaka 2013 ukihusisha vijiji 5 ambavyo ni Kimbo, Shembekeza, Mashewa, Bombani na Kwaisaka ukiwa na wanachama 473 na hadi Juni 2016 UWAMAKIZI ulikuwa na jumla ya wanachama 610 kutoka vijiji 8 vya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.

  [caption id="attachment_6271" align="aligncenter" width="1000"] Mtaalam wa Mazingira na Afisa Ubora na Viwango Ramadhan Nyambukah akielezea jambo wakati wa mkutano baina ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo (hayupo pichani) na wandishi wa habari mapema hivi karibuni Ofisini kwake kuhusu mafanikio yatokanayo na utafiti kupitia Filamu ya Mamba wa Zigi. Filamu hiyo imeelezea namna wananchi wanaozunguka maeneo ya mto Zigi unaounganisha wilaya za Muheza, Mkinga na Tanga wanavyoathiriwa na uharibifu wa vyanzo vya maji.[/caption]

Mhandisi Mgeyekwa anasema kutoka mwaka 2013-2016, TANGA UWASA kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imeupatia Umoja huo kiasi cha Tsh. Milioni 100 kwa ajili ya kuendesha elimu ya kilimo hai na kilimo hifadhi sambamba na kampeni ya uhamasishaji wa uhifadhi wa mazingira.

Anasema hadi kufikia Juni 2017 kupitia juhudi za Umoja huo, jumla ya miti 3,196,174 imeoteshwa na kupandwa katika maeneo yote yanayozunguka vijiji vilivyopo ndani ya mradi ikihusisha miti ya mbao, matunda, viungo na miti rafiki na maji.

Akifafanua zaidi Mhandisi Mgeyekwa anasema kupitia utafiti wa filamu mwaka 2016, Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) zimeanza utekelezaji wa mradi wa miaka (2016-2020) wa uhifadhi wa mazingira katika Bonde la Mto Wami na Bonde la Mto Zigi.

[caption id="attachment_6274" align="aligncenter" width="1000"] Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima Wahifadhi Mazingira Kihukwi Zigi (UWAMAKIZI) Twaha Rajab Mbarook akitoa ufafanuzi namna Filamu ya Mamba wa Zigi ilivyowasaidia kuibua mradi wa utunzaji mazingira na uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa kutumia kilimo cha kisasa mapema hivi karibuni Jijini Tanga. Kutoka kushoto ni Katibu wa UWAMAKIZI Bw. Simon Mnzava na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya National Historical Documentation and Film Production ambao ndiyo watengenezaji wa Filamu hiyo Bw. Humphrey Mgema.[/caption]

Anaongeza kuwa mradi huo umetengewa kiasi cha Tsh. Milioni 180, ambapo mpaka sasa kiasi cha Tsh. Milioni 80 zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo ikiwemo kutandaza mabomba na kufunga viunganishi kwa ajili ya kusambaza maji kwa wananchi waliopo katika vijiji vya Mashewa, Kimbo na Shembekeza waliopo katika umbali wa kiomita 2.5 kati ya kilometa 6.5 zinazohitaji.

“Mradi huu pia utasaidia kujenga malambo ya kunyweshea mifugo katika eneo la Bwawa la Mabayani ili kuzuia mifugo kunywa maji moja kwa moja kutoka Mto Zigi, ambapo kaisi cha Tsh. Milioni 50 tayari zimetengwa” anasema Mgeyekwa.

Sote tunafahamu kuwa asilimia 75 ya uso wa dunia ni maji na asilimia 70 mpaka 75 ya mwili wa binadamu pia inachukuliwa na maji, kuhakikisha kuwa utunzaji na uendelezaji wa rasilimali za maji unaendelezwa kwa ushirikiano na mipango ya pamoja.

[caption id="attachment_6275" align="aligncenter" width="1000"] Picha ikionyesha moja ya bango ambalo ni moja ya nyenzo ambayo inatumika kuhamasisha jamii ili iweze kutunza na kuhifadhi mazingira. Bango hilo limewekwa na Umoja wa Wakulima Wahifadhi wa Mazingira Kihukwe Zigi (UWAMAKIZI) katika maeneo ya vijiji vya Mashewa, Kimbo na Shembekeza Wilayani Muheza Mkoani Tanga. Umoja huo unafadhiliwa na TANGA UWASA katika kuhakikisha inalinda vyanzo vya maji vilivyopo.

[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi