Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kutafuta mbinu bora za kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini ili kukuza sekta hiyo.
Amesema licha ya Tanzania kuwa na vivutio vingi vya utalii lakini idadi ya watalii wanaoingia nchini kwa mwaka ni ndogo, hivyo kuna haja ya kuboresha matangazo.
Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumatano, Agosti 23, 2017) wakati alipofanya ziara katika mji wa kitalii wa Varadero ulioko kwenye mkoa wa Matanzas nchini Cuba.
Alisema mji wa Varadero tu unaingiza watalii zaid...
Read More