Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Miradi ya Maji Ruvu Juu na Ruvu Chini Kupunguza Tatizo la Maji Dar
Aug 29, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_10857" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Mhandisi Romanus Mwang’ingo, akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Rodney Thadeus. (Picha na Fatma Salum).[/caption]

Na: Neema Mathias & Agness Moshi

Imeelezwa kuwa kukamilika kwa miradi ya maji ya Ruvu juu na Ruvu chini kutasaidia kupunguza tatizo la maji kwa asilimia 74 kwa wakazi wa Dar es Salaam ambao walikua na upungufu maji wa takribani lita millioni 244 kwa siku.

Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam Leo na Kaimu  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Dar es Salam (DAWASA) Eng.Romanus Mwangingo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na mamlaka hiyo.

Alisema katika kipindi cha miaka miwili iliyopita Mkoa wa Dar es Salam  ulikuwa unapata maji lita Milioni 300 kwa siku ambazo zilikua hazitoshelezi mahitaji kwasabubu mahitaji ya wastani kwa siku ni  lita millioni 544.

 Kuongezeka kwa uzalishaji katika mitambo ya  Ruvu Juu na Ruvu Chini imeongeza kiwango cha uzalishaji maji na uwezo wa kuzalisha maji  kwa siku nilita million 502 jambo ambalo limesaidia sana upatikanaji wa maji katika maeneo mengi ya Jiji.

“lengo letu ni kufikia asilimia 95 ya upatikanaji wa maji ifikapo mwaka 2020, tunaendelea na utekelezaji wa maradi wa uchimbaji wa visima vya Mpera na Kimbiji ambavyo vitaongeza maji lita million 260 na ukijumlisha na idadi tuliyonayo tutafikisha lita million 756 kwa siku ambayo itatosheleza mahitaji hadi kufikia mwaka 2027,” alibainisha Eng Romanus.

Pia Eng. Romanus alieleza katika mradi wa upanuzi wa mitambo ya mradi wa Ruvu Juu na Ruvu Chini wana mpango wa kujenga bwawa la Kitunda ili kuhifadhi maji yatokanayo na mvua kwa matumizi ya wakazi wa Jiji na mradi huo utaongeza lita million  180 hadi 270.

DAWASA pia imeanza utekelezaji wa mradi wa ukusanyaji na uondoaji wa majitaka ambapo wanatarajia kuyasafisha maji hayo ili hatimaye yaweze kutumika tena.

“Mradi huu unahusisha ujenzi wa mitambo mitatu mikubwa ya kisasa ya kusafisha majitaka itakayokwenda sambamba na ulazaji wa mabomba ya kukusanya maji taka ambayo itajengwa Jangwani, Mbezi Beach na Kurasini ili kuongeza kiwango cha kusafisha majitaka cha 10% kwa sasa hadi  kufikia 30% ifikapo mwaka 2020,”alifafanua Eng  huyo.

 Alisema mradi huo unaojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Korea kupitia mkopo wa masharti nafuu ya benki ya Exim ya Korea na unatarajiwa kugharimu takribani dola za Kimarekani Milioni 90 ambazo tayari zimepatikana.

Pamoja na kuelezea mafanikio hayo Mhandisi Mwangingo amesema DAWASA bado inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa fedha za kutosha ili kuweza kusambaza na kuzalisha maji ya kutosha kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, pamoja na kuondoa na kusafisha maji taka, hivyo akaiomba serikali pamoja na Wizara ya Maji kuona jinsi watakavyowasaidia.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi