SERIKALI YASITISHA UTOAJI WA MAENEO MAPYA YA UTAWALA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imesitisha zoezi la kutoa maeneo mapya ya utawala hadi itakapotangazwa vinginevyo.
"Kwa sasa tumesitisha kutoa maeneo mapya ya utawala ili tuimarishe kwanza yale ya awali. Tunaimarisha kwanza miundombinu ya majengo ya ofisi, nyumba za watumishi kwenye wilaya na Halmashauri mpya, zikitengamaa tutafanya maamuzi mapya, " alisema.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Ijumaa, Agosti 11, 2017) katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Ulyankulu na Kaliua...
Read More