[caption id="attachment_10825" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus (kulia) akipokea cheti cha heshima toka kwa Afisa Uhusiano wa Kampuni ya SportPesa Bi. Sabrina Msuya cha kutambua mchango wa Idara ya Habari (MAELEZO) katika kufanikisha uratibu wa vyombo vya habari wakati wa ujio wa timu ya Everton hapa nchini mapema mwezi Julai Mwaka huu.[/caption]
Na: Paschal Dotto
Katika kutambua utendaji kazi wa idara ya habari(MAELEZO) kampuni inayojishughulisha na mchezo wa kubashiri ya Sportpesa leo imetoa Cheti cha Shukrani kwa Idara hiyo kwa kushiriki vizuri katika ujio wa timu ya Everton nchini Julai mwaka huu.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bw.Rodney Thadeus aliishukuru kampuni hiyo kwa kutambua kazi nzuri ya Idara ya Habari (MAELEZO) kuanzia kuwasili kwa timu hiyo kwa kuweka mazingira mazuri ya waandishi wa habari.
Idara ya Habari ilifanya maandalizi na uratibu wa vyombo vya habari kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, uwanja wa taifa wakati timu ya Everton inafanya mazoezi pamoja na siku mchezo wao dhidi ya Gor Mahia.
“Kwa mazingira yale ya wachezaji wakubwa huwa wanahitaji sana usalama kwa hiyo mtu yeyote ambaye anataka kwenda kuchukua habari lazima awe ametambuliwa na Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) na jukumu hilo tulilitekeleza kikamilifu kuhakikisha kwamba hakuna mwandishi ambaye atazuiliwa kuingia uwanjani”, alisema Bw.Rodney.
Bw. Rodney alisema kwamba sportpesa wametambua kuwa kuna Idara ya Habari (MAELEZO) na kutambua kwao inaonyesha jinsi gani Idara hii kuanzia kwa Mkurugenzi mkuu, Wakurugenzi wasaidizi pamoja na maofisa wake wanafanya kazi inayotambulika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
[caption id="attachment_10828" align="aligncenter" width="750"] Cheti cha Heshima ilichopata Idara ya Habari (MAELEZO) toka Kampuni ya SportPesa kwa kutambua mchango wa Idara hiyo katika kufanikisha uratibu wa vyombo vya habari wakati wa ujio wa timu ya Everton mapema Julai Mwaka huu.Aidha Bw. Rodney alisema tuzo hiyo itakuwa ni chachu ya kuendelea kufanya kazi kwa kasi zaidi katika Idara hiyo ili kazi za Idara ziweze kufahamika zaidi, lakini kubwa zaidi ni kuizungmzia Serikali na kazi zake katika Nyanja zote kuanzania kwenye michezo na maeneo mengine ya uchumi, siasa pamoja na biashara.
Kwa uapande wake Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo Bi. Sabrina Msuya aliishukuru Idara ya Habari (MAELEZO) kwa kazi nzuri wanayoifanya hususani kutoa ushirikiano katika kufanikisha shughuli hiyo ya ujio wa timu ya Everton.
“Tunaishukuru Idara ya Habari (MAELEZO) kwa kutupa ushirikiano wenu kufanikisha shughuli nzima ya Everton kuanzia wanakuja, wakati wa mechi mpaka wanaondoka huu ni mwanzo mzuri na tuanomba ushirikaiano wenu katika kuendeleza soka Tanzania “, alisema Bi. Msuya.
Wakati wa ujio wa timu ya Everton Idara ya Habari(MAELEZO) ikishirikiana na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) ilihakikisha kila mwandishi anatekeleza majukumu yake ya kihabari licha ya vibali vya waandishi kuisha jambo ambalo liliwezekana.