Na Shamimu Nyaki - WUSM
Mkurugenzi Msaidizi Lugha, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Resan Mnata ametoa wito kwa Wadau wa Utamaduni kujitokeza kufadhili na kuunga mkono shughuli za Utamaduni nchini.
Dkt. Mnata ametoa rai hiyo Julai 23, 2022 Chamwino Dodoma, wakati wa Tamasha la 13 la Muziki wa Cigogo katika Kijiji Cha Chamwino Ikulu.
Aidha, Dkt. Mnata ametoa pongezi kwa Dkt. Kedmon Mapana, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambaye ndiye mwanzilishi wa Tamasha hilo ambalo limesaidia kueneza na kukuza Mila...
Read More