Rais Mhe. Samia Ashiriki Siku ya Ufungaji wa Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya EAC Jijini Arusha
Jul 23, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Rais wa Burundi, Mhe. Évariste Ndayishimiye akizungumza mara baada ya kuchaguliwa katika siku ya mwisho ya Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) tarehe 22 Julai, 2022.
Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) aliyemaliza muda wake, Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais wa Burundi, Mhe. Évariste Ndayishimiye mara baada ya kuchaguliwa katika Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) tarehe 22 Julai, 2022.