Rais Mhe. Samia na Rais Kenyatta Wafungua Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki
Jul 22, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye pamoja na viongozi wengine wakivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) katika Sherehe zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Burundi, Mhe. Évariste Ndayishimiye pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) katika Sherehe zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta wakati wa Sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022.
Kwaya ya Utumishi ikitoa burudani katika Sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022.
Muonekano wa Barabara ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) ambayo imefunguliwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta katika Sherehe zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022.