Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (kushoto) ambaye anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Marrakech, nchini Morocco, kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, ambaye pia ni Gavana mbadala wa Tanzania katika Benki ya Dunia, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakielekea kwenye Mkutano wa 26 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika ambazo ni wanachama wa Benki ya Dunia.
Read More