Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tamasha la Wamatengo Sasa Kufanyika Kila Mwaka
Oct 31, 2023
Tamasha la Wamatengo Sasa Kufanyika Kila Mwaka
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiangalia baadhi ya bidhaa kabla ya kufungua tamasha hilo katika kijiji cha Makumbusho Mtama, wilayani Mbinga.
Na Shamimu Nyaki

Tamasha la Utamaduni wa kabila la Wamatengo mkoani Ruvuma litafanyika kila mwaka ili kutangaza utamaduni wa kabila hilo na Mkoa wa Ruvuma ndani na nje ya Tanzania.

Hayo yameelezwa Oktoba 30, 2023 na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati akifungua tamasha hilo katika kijiji cha Makumbusho Mtama, wilayani Mbinga.

"Matamasha haya yanatangaza Utamaduni, Mila na Desturi zetu Watanzania, tamasha hili lifanyike kila mwaka ili kukumbushana maisha yetu ya asili, na nitoe rai kwa makabila mengine kuwa na Matamasha kama haya katika maeneo yao," amesema Mhe. Dkt. Ndumbaro.

Tamasha hilo lilishereheshwa na burudani mbalimbali  na kupambwa na  maonesho ya tamaduni zenye asili ya kabila hilo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi