Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Mobhare Matinyi atembelea Makao Makuu ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) jijini Dodoma ambapo amekutana na Bw. James Mloe, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko huo.
Bw. Matinyi ametembelea PSSSF kwa lengo la kujifunza na kuelewa shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.
Aidha, hili ni zoezi endelevu ili kuweza kupata taarifa mbalimbali za kimaendeleo na mafanikio ya PSSSF kwa lengo la kuisemea Serikali na kuwafikia watanzania.