[caption id="attachment_46955" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akiongoza kikao cha menejimenti ya wizara yake kinachofanya ukumbi wa wizara jijini Dodoma kuhusu maandalizi ya sera mpya ya kilimo ya mwaka 2019.[/caption]
Waziri wa Kilimo Japheti Hassunga leo amekutana na Menejimenti ya wizara, wakuu wa Taasisi na Wenyeviti wa Bodi za Mazao zilizopo chini ya Wizara.
Lengo la mkutano huu wa siku mbili unaofanyika katika ukumbi wa wizara Jijini Dodoma ni kujadili maandalizi ya sera mpya ya kilimo ya mwaka 2019 na kuondoa mapungufu yaliopo katika sera ya mwaka 2013.
Akiongea katika kikao kazi hicho Waziri Hasunga ameeleza umuhimu wa kuwa na sera mpya ya kilimo ni kufanya kilimo kuwa na tija na cha kibiashara, hivyo kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya kilimo
“Tunataka sera mpya ya kilimo ilenge kukifanya kilimo kuwa shughuli kuu ya kiuchumi itakayochangia kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira” alisisitiza Waziri Hasunga.
Waziri Hasunga amebainisha kwamba sera mpya inatakiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu ili kutoa fursa kwa Bunge kutunga sheria na kanuni za kilimo.
Aidha katika mkutano huu wizara ya kilimo itajadili na kupitia taarifa ya utekelezaji wa shughuli kwa mwaka 2018/2019 na kuweka mkakati madhubuti wa utekelezaji mipango utendaji kazi ya wizara kwa mwaka 2019/2020.
Kikao hicho kinahudhuriwa na Manaibu Waziri Hussein Bashe na Omary Mgumba, Katibu Mkuu Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu Profesa. Siza Tumbo.