Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Ashiriki Uzinduzi wa Global Africa Investment Summit
Feb 04, 2026
Rais Samia Ashiriki Uzinduzi wa Global Africa Investment Summit
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki uzinduzi wa Global Africa Investment Summit (GAIS) jijini Dubai.
Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki uzinduzi wa Global Africa Investment Summit (GAIS) jijini Dubai, tukio lililoashiria hatua mpya ya Afrika katika kuvutia mitaji ya kimataifa kupitia uwekezaji uliopangiliwa na wenye uhalisia wa kifedha.

Akihutubia mkutano huo, usiku wa Februari 3, Mhe. Rais Samia alisisitiza kuwa wawekezaji hawatafuti fursa pekee, bali uaminifu, uthabiti wa sera, taasisi imara na serikali zinazotekeleza ahadi zake.

Alieleza namna Tanzania ilivyowekeza kimkakati katika nishati, reli, bandari na miundombinu ya uchukuzi, pamoja na maeneo  maalum ya uwekezaji na diridha moja la uwekezaji, ili kujenga mazingira rafiki kwa wawekezaji wa muda mrefu.

Ushiriki wa Tanzania katika GAIS unaakisi dhamira ya nchi ya kwenda kwenye ushirikiano uliopangiliwa vizuri na unaoendana na vipaumbele vya maendeleo ya taifa na matarajio ya wawekezaji wa kimataifa.

GAIS inalenga kuoanisha uongozi wa kisiasa, rasilimali za kitaifa na mitaji ya kimataifa, na kuifanya Afrika, hususan Tanzania kuwa kitovu cha uwekezaji unaoleta matokeo, ajira na maendeleo endelevu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi