Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Arusha mjini, Mhe. Paul Makonda amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika jiji la Arusha ikiwa ni utekelezaji wa ahadi za serikali na kuimarisha miundombinu katika kipindi hiki ambacho Arusha itakuwa katika Mashindano ya AFCON 2027.


Mhe. Makonda amefanya ziara hiyo tarehe 3 Februari, 2026 ambapo alikagua miradi ya miundombinu, huduma za kijamii na maendeleo iliyopo maeneo ya Arusha mijini.

Makonda pia alijikita kwenye ukaguzi wa sekta mbalimbali za miundombinu ikiwemo ujenzi wa Stendi ya mabasi ya mkoa wa Arusha, ujenzi wa Soko la Kilombero na ujenzi wa jengo jipya la Halmashauri ya jiji la Arusha