Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wilaya ya Nyasa  Kukamilisha Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Kwa Muda Uliopangwa
Jun 04, 2019
Na Msemaji Mkuu

 

Na Netho Credo- Nyasa

Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashuri ya  Wilaya  ya Nyasa mkoani Ruvuma Jimson Mhagama amesema kuwa atahakikisha  ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo  unakamilika kabla ya Juni 30 mwaka huu kama ilivyopangwa.

Ameyasema hayo leo wakati akiongea na mwandishi wa habari  Ofisini kwake kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayoendelea kujengwa katika Kijiji cha Nangombo ambapo  moja ya hatua alizochukua ni kuhamisha vikao vyote vya wakuu wa Idara na Vitengo kufanyika katika eneo la mradi huo.

Mhagama alifafanua kuwa amelazimika kubadili eneo la kufanyia vikao vya wakuu wa Idara Wilayani hapa  kutoka Ofisini kwake  hadi kufanyia eneo la Ujenzi wa Hospitali katika kijiji cha Nangombo kwa lengo la kuongeza ufanisi wa kazi ili kila mkuu wa idara aone kwa macho maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya mpaka itakapokamilika.

” Lengo la Serikali ni kutatua kero ya wananchi wa Wilaya ya Nyasa waliokuwa wakitembeai umbali wa kilomita 66 kufuata huduma za matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya mbinga”

Aliongeza kuwa vikao vyote vya wakuu wa idara alivyokuwa akivifanya Ofisini kwake sasa amevihamishia katika eneo la ujenzi na kila mkuu wa idara na Vitengo wanatakiwa kushiriki bila kukosa mpaka juni 30 tutakapokuwa tumeshakamilisha ujenzi huu wa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa.

“kuanzia leo vikao vyote vya kiutawala vinavyojumisha Wakuu wa idara na Vitengo vitakuwa vinafanyika katika eneo la Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa katika Kijiji cha Nangombo kata ya kilosa na kila Mkuu wa idara na Vitengo wanatakiwa kufika bila kukosa wala kuchelewa. Mheshimiwa Rais amezitoa fedha hizi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huu kwa wakati tuna kila sababu ya kusimamia ujenzi huu kwa nguvu zote” alisema Mhagama.

Aidha, katika hatua nyingine amempongeza sana Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kuwajali wananchi wa Wilaya ya Nyasa kwa kuwapa fedha ya kujengea Hospitali ya Wilaya ya Nyasa kwa kuwa walikuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za matibabu.

Aidha, Mhagama alitoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa kutembelea na kuona jinsi ujenzi unavyoendelea na kutoa maoni na ushauri kwa kuwa Hospitali hii ni mali ya wana Nyasa.

   

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi