Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wenye Hatari ya Kujifungua Watoto Wenye Magonjwa ya Moyo Washauriwa Kufanya Vipimo.
Sep 11, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_13095" align="aligncenter" width="750"] Daktari Bingwa wa Magonjwa Moyo kwa Watoto Dkt.Naiz Majani akielezea umuhimu wa akina mama wajawazito kufanya kipimo cha‘Fetal Echocardiography’ katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii mapema hivi karibuni. Kipimo hicho ni maalum kwa ajili ya kupima wajazito ili kubaini kama watoto waliotumboni wana ugonjwa wa moyo.[/caption]

Na: Agness Moshi 

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imewashauri wajawazito walio kwenye hatari ya kujifungua watoto wenye magonjwa ya moyo kufanya kipimo cha‘Fetal Echocardiography’ ili waweze kugundua tatizo mapema na kulipatia tiba.

Akiongea na waandishi wa habari katika mahojiano maalum,Daktari Bingwa wa Magonjwa  Moyo kwa  Watoto Dkt.Naiz Majani amesema  ni vyema wajawazito walio kwenye hatari ya kujifungua watoto wenye magonjwa ya moyo kuhakikisha wanafanya kipimo hicho mapema  ili kujua hali ya mtoto tumboni  kufanya kipimo cha magonjwa hayo  ili kuweza kugundua tatizo mapema na kujiandaa kukabiliana nalo.

Dkt.Naiz  alitaja baadhi ya wajawazito walio kwenye hatari ambao ni pamoja na  waliowahi kuzaa mtoto mwenye tatizo la moyo,wanaotumia dawa za muda mrefu kama vile dawa za kifafa,wenye mimba ya mapacha ,wanaougua  ugonjwa wa kisukari, wenye mgonjwa wa moyo kwenye familia zao au ambao kwenye vipimo walivyofanya wamekuta mtoto anatatizo lolote.

 “Magonjwa mengi ya moyo ya kuzaliwa yanatibika lakini yanasharti kubwa la kujulikana mapema na yanahitaji tiba kwa wakati muafaka, inaumiza  sana unapogundua mtoto anatatizo la moyo halafu unamwambia hatuwezi kufanya upasuaji kwa sababu tu amechelewa”, alisema Dkt.Naiz.

Dkt.Naiz alisema kuwa kuna wakati mtoto anagundulika na tatizo lakini anashindwa kufanyiwa upasuaji si kwasababu hakuna tiba bali kwasababu amefika kliniki ya moyo kwa wakati usiosahihi kwa upasuaji, hivyo  ni vyema kwa mjamzito kuwahi kufanya kipimo ili aweze kumsaidia mtoto  kupata tiba kwa wakati.

[caption id="attachment_13096" align="aligncenter" width="750"] Daktari Bingwa wa Magonjwa Moyo kwa Watoto Dkt.Naiz Majani akielezea umuhimu wa akina mama wajawazito kufanya kipimo cha‘Fetal Echocardiography’ katika mahojiano maalum na waandishi wa habari mapema hivi karibuni. Kipimo hicho ni maalum kwa ajili ya kupima wajazito ili kubaini kama watoto waliotumboni wana ugonjwa wa moyo. (Picha na Idara ya Habari - MAELEZO)[/caption]

“ Kuna magonjwa ya moyo yanatakiwa yatibiwe ndani ya mwezi baada ya kuzaliwa,mengine ndani ya miezi sita au mwaka mmoja inategemea na tatizo alilonalo mtoto, hivyo  kwa kufanya kipimo cha Fetal Echocardiography tutaweza kugundua  tatizo la mtoto mapema angali akiwa tumboni mwa mama na  kujiandaa na matibabu kwa muda muafaka”,alisema Dkt.Naiz.

Aidha, Dkt.Naiz amesema kuwa kipimo hicho ni salama kwa mama na mtoto kwasababu hakina mionzi ambayo ingeleta  madhara na kinafanya kazi  kwa  mimba ya umri wowote japo inapendeza zaidi  mimba ifikishe walau miezi  minne hadi saba  kwa sababu kwa wakati huo  tatizo linaonekana vizuri.

“Kipimo cha Fetal  Echocardiography ni ‘ultrasound ‘ ambayo inapima magonjwa ya moyo kwa mtoto aliye tumboni hivyo wajawazito wasiwe na wasiwasi wowote kwa sababu hakina utofauti na ultrasound aanazofanya wakati wa ujazito”,alisisitiza Dkt.Naiz.

Hata hivyo, Dkt.Naiz amesema si lazima mjamzito mwenye hatari ya kujifungua mtoto mwenye ugonjwa wa moyo ndio anatakiwa apime hata wasio kwenye hatari wanakaribishwa  kufanya kipimo hicho kwa tahadhari kwani  tafiti  zinaonyesha mtoto mmoja kati ya 100 huzaliwa na ugonjwa wa Moyo hivyo ni vyema kujua hali ya mtoto mapema kwasababu mtoto wa yeyote anaweza kuzaliwa na tatizo.

Kwa sasa ,huduma hii inapatikana kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) pekee  na tayari wajawazito 35 wamefanyiwa ambapo   watano kati yao wamegundulika na tatizo na tayari maandalizi ya matibabu yao yameanza.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi