Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mhagama Akerwa na Sekta Binafsi ya Ulinzi Kuongoza kwa Migogoro Mahala pa Kazi
Jan 15, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_39766" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongea, wakati wa kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (hawapo pichani) kilichowakutanisha Wasuluhishi na waamuzi wa migogoro ya kikazi nchi nzima, mjini Morogoro, tarehe 14 Januari, 2019.[/caption]

Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ameiagiza Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, kuweka mpango Maalum wa kuhakikisha migogoro   katika sekta  binafsi ya Ulinzi haizalishwi tena kwa wingi kwani inasababisha kutumika vibaya kwa rasilimali muda kati ya mwajiri na Mfanyakazi hali inayopelekea kuchelewesha Maendeleo.

Waziri Mhagama amebainisha sekta  nyingine zinazoongoza kuwa na migogoro mahala pa kazi   kuwa ni  Sekta  ya Ujenzi na Sekta  ya Elimu. Aidha, ameitaka Tume hiyo kufanya utafiti kwa sekta   zote zinazoongoza kwa migogoro ya kikazi ili kubaini chanzo cha migogoro hiyo na kuandaa Mkakati Maalum wa kuishughulikia.

[caption id="attachment_39767" align="aligncenter" width="900"] Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, Shanes Nungu akiongea, wakati wa kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kilichowakutanisha Wasuluhishi na waamuzi wa migogoro ya kikazi nchi nzima, mjini Morogoro, tarehe 14 Januari, 2019.[/caption]

Mhagama ameyasema hayo leo mjini Morogoro  tarehe 14 Januari,  2019, wakati wa kikao cha Baraza la  wafanyakazi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kilichowakutanisha Wasuluhishi na  waamuzi wa migogoro ya kikazi nchi nzima.

"Hii sekta  Binafsi ya Ulinzi kwa nini huko migogoro  haiishi? Nataka mpango wa kumaliza migogoro hiyo, shirikianane na Taasisi nyingine muweke mpango maalum utakao weza kutatua na kuhakikisha haizalishwi mogogoro  mingine" Alisisitiza Mhagama.

[caption id="attachment_39768" align="aligncenter" width="900"] Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi wakiwa katika kikao hicho kilichowakutanisha Wasuluhishi na waamuzi wa migogoro ya kikazi nchi nzima, mjini Morogoro, tarehe 14 Januari, 2019.[/caption]

Mhagama alifafanua kuwa Serikali ya Awam  ya Tano  inayoogozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiriakwa vitendo vya kupiga vita uzembe, ubadhirifu na vitendo vyote  Vya rushwa mahala  pa kazi.

  "Nisisitize kazi ya Usuluhishi na Uamuzi ni  kazi ya heshima na pia ni  kazi ya wito. Hivyo wekeni mkazo kwenye suala la Usuluhishi ili kupunguza muda  na mlundikano wa  mashauri, pia bainisheni sekta  nyingine zenye migogoro  mikubwa. Elimu ni  vyema iendelee kutolewa kwa Wadau kuhusu Sheria za Ajira na mahusiano kazini." alieleza Mhagama.

Awali akiongea katika Mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, Shanes Nungu alibainisha kuwa Tume hiyo itatekeleza maagizo hayo kwa kuboresha Mkakati Wa Mpango kazi Wa Tume ili kuwa na mpango mkakati kwenye mtazamo Wa kupunguza migogoro  na unaolenga kumaliza migogoro kwa nataka katika sekta  zinazoongoza kuwa na migogoro mahala  pa kazi.

 "Tumekuwa tunajitahidi kumaliza na kuipunguza migogoro ya kikazi, kwani tumefanikiwa kumaliza migogoro hiyo kwa asilimia 80 kwenye hatua ya Uamuzi na asilimia 77, kwenye hatua ya Usuluhishi" alieleza Nungu.

Tume ya Usuluhishi na Uamuzi  ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambapo  Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume hiyo kimefanyika kwa mujibu wa Agizo la Rais Na.1 la mwaka 1970. Baraza hilo   huiwezesha Tume kuboresha Huduma na masuala ya utatuzi Wa migogoro ya kikazi kwa njia ya Usuluhishi na Uamuzi.

 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi