Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yaimarisha Mafunzo kwa Vijana Kupitia VETA
Feb 16, 2026
Serikali Yaimarisha Mafunzo kwa Vijana Kupitia VETA
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), CPA Anthony Kasore akizungumza na waandishi wa habari kuhusu miradi ya maendeleo na fursa kwa vijana katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mtumba jijini Dodoma.
Na Naishooki Makeseni - MAELEZO

Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuimarisha sekta ya elimu ya ufundi stadi kwa kuelekeza nguvu katika kuwawezesha vijana kuunda ajira kupitia ujuzi badala ya kusubiri kuajiriwa.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), CPA Anthony Mzee Kasore, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mtumba jijini Dodoma.

CPA Kasore amesema mageuzi yanayoendelea katika ufundi stadi ni mapinduzi yanayolenga kubadili maisha ya vijana na kuimarisha uchumi wa Taifa akieleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Novemba 14, 2025 wakati wa akifungua Bunge la 13, alisisitiza kuweka kipaumbele kwa sera na programu zitakazopanua fursa za kiuchumi na ajira kwa vijana.

nnn.                      
Amesema kwa sasa VETA ina vyuo 80 vinavyohudumia zaidi ya wanafunzi 86,000 kwa mwaka. Serikali inalenga kuongeza vyuo hivyo hadi 152 ifikapo mwaka 2027 na kuongeza udahili hadi wanafunzi 250,000 kwa mwaka.

Ameongeza kuwa Serikali tayari imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 100 kujenga vyuo vipya vya ngazi ya wilaya kote nchini, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha kila kijana anapata fursa ya kujifunza ujuzi karibu na makazi ya watu.

CPA kKasore amebainisha kuwa hatua hiyo ni sehemu ya safari ya kujenga “Tanzania Mpya” yenye vijana wenye ujuzi, wabunifu na wenye uwezo wa kuchochea maendeleo ya Taifa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi