[caption id="attachment_40935" align="aligncenter" width="1000"] Rais wa Shirikisho la Viwanda vya Misitu Tanzania ( SHIVIMITA) Ben Sulus akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu kuhusu kuongezewa muda wa mikataba kutoka miaka miwili hadi miaka mitano ya kupewa vitalu vya miti katika Shamba la Miti la Sao Hill lililopo mkoani Iringa wakati Washirika hao walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.[/caption]
Na Lusungu Helela-WMU
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii. Mhe. Constantine Kanyasu amewahakikishia wamiliki wa viwanda vya misitu Tanzania kuwa atashughulikia ombi lao la kutaka kuongezewa muda wa mikataba yao kutoka miaka miwili hadi mitano ya kupewa mgao wa vitalu vya miti
Pia ameahidi kuyafanyia kazi malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa ofisini kwake na wamiliki hao yakiwemo ya gharama za tozo ya ushuru wa mazao ya misitu (Cess) inayotozwa na Halmashauri za wilaya ya Mufindi ambayo licha Serikali kutoa maagizo ya kuzuia tozo hiyo bado wadau hao wanaendelea kutozwa.
[caption id="attachment_40933" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akisalimia na baadhi ya Wanachama wa Shirikisho la Viwanda vya misitu Tanzania mara baada ya kufanya mazungumzo nao kuhusu ombi la kuongezewa muda wa mikataba kutoka miaka miwili hadi miaka mitano ya kupewa vitalu vya miti katika Shamba la Miti la Sao Hill lililopo mkoani Iringa wakati Washirika hao walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma[/caption]Mhe. Kanyasu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Rais wa Shirikisho la Viwanda vya Misitu Tanzania (SHIVIMITA) na Wanachama wa Shirikisho hilo waliomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.
Katika mazungumzo hayo, Rais wa SHIVIMITA, Ben Sulus amemuomba Naibu Waziri aangalie namna ya kuwasaidia wadau hao waongezewe muda wa mikataba kutoka miaka miwili hadi mitano ya kupewa mgao wa vitalu vya misitu ili waweze kupata mikopo kutoka kwenye Taasisi za Kifedha kwa ajili ya kuendeshea viwanda vyao
Rais huyo ameeleza kuwa Taasisi za Kifedha zimekuwa zikiwanyima mikopo kwa kuhofia fedha zao kupotea kutokana na wadau hao kutokuwa na uhakika wa kuongezewa mikataba mara baada ya mikataba yao ya kuvuna magogo ya miaka miwili waliyopewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS).
Amesema endapo watapewa mikataba ya miaka mitano watakuwa na uhakika wa kuweza kuendeleza viwanda vyao kwa vile Taasisi hizo za Kifedha zitaweza kuwapa mikopo watakayoomba na zitakuwa na uhakika wa kurudishiwa fedha hizo.
Katika hatua nyingine, Wadau hao wamemuomba awe mlezi wao katika jitihada wanazozichukua za kuhakikisha wanakuwa wazalishaji wa bidhaa za mwisho kama vile milango pamoja na meza zitokanazo na mbao badala ya kujikita kuuza mbao tu.