Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Kabudi Akabidhiwa Uenyekiti wa Mawaziri wa SADC
Aug 13, 2019
Na Msemaji Mkuu

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto) akipokea ngao kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia Nemtumbo Nandi ikiwa ni ishara ya kuupokea uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi akitoa hotuba yake mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) iliyofanyika mapema leo Agosti 13, 2019 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
Baadahi ya Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wanaoshiriki mkutano wa 39 wa jumuiya hiyo unaofanyika Jijini Dar es Salam wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Tanzania kukabidhiwa Uenyekiti wa baraza hilo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi