Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Jafo awaagiza Wakurugenzi kuwawezesha Maafisa Michezo kushiriki vikao kazi.
Dec 13, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_49812" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akizungumza na Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara waliohudhurua Kikao Kazi cha siku mbili (12 – 13,Desemba 2019) kilichoongozwa na Kauli Mbiu “Michezo kwa Afya,Ajira na Maendeleo ya Viwanda” wakati akifunga kikao hicho leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_49813" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akizungumza na Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara waliohudhurua Kikao Kazi cha siku mbili (12 – 13,Desemba 2019) kilichoongozwa na Kauli Mbiu “Michezo kwa Afya,Ajira na Maendeleo ya Viwanda” wakati akifunga kikao hicho leo Jijini Dodoma.[/caption]

Na Anitha Jonas – WHUSM, Dodoma

13/12/2019.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo amewaagiza wakurugenzi wote wa Halmashauri kuhakikisha wanawawezesha Maafisa Michezo katika ofisi zao kushiriki katika kikao cha mwakani.

Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo jijini Dodoma alipokuwa akifunga Kikao kazi cha Maafisa Michezo wa Tanzania Bara ambacho kimefanyika kwa mara ya kwanza jijini Dodoma kikilenga kuwajengea uwezo maafisa hao katika kusimamia masuala ya michezo na kujitathmini na kupeana maelekezo ya nini kifanyike kuboresha sekta ya michezo nchini.

“Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 imejadili kwa upana agenda ya michezo na kwa kiongozi yoyote wa serikali anayepinga suala la michezo ni mmoja ya watu wanaokwamisha utekelezaji wa ilani kwani watumishi wa umma wanatekeleza ilani ya chama kilichopo madarakani,’alisema Mhe.Jafo.

[caption id="attachment_49814" align="aligncenter" width="1000"] Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi akitoa taarifa fupi ya kikao kazi cha Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara kilichofanyika kwa siku mbili (12 – 13,Desemba 2019) wakati wa ufungaji wa kikao hicho uliofanywa na Mhe. Selemani Jafo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Jijini Dodoma kilichoongozwa na Kauli Mbiu “Michezo kwa Afya,Ajira na Maendeleo ya Viwanda"[/caption] [caption id="attachment_49815" align="aligncenter" width="975"] Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Bernard Patrick akitoa ufafanuzi kuhusu Muundo wa Utumishi katika kada ya Michezo kwa Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa siku mbili (12 – 13,Desemba 2019)kilichoongozwa na Kauli Mbiu “Michezo kwa Afya,Ajira na Maendeleo ya Viwanda” leo Jijini Dodoma.[/caption]

Akiendelea kuzungumza wakati wa kufunga kikao kazi hicho Mhe.Jafo alisisitiza hivi karibuni baada ya michezo kurudishwa mashuleni tumeshuhudia vijana wadogo wakifanya mambo makubwa katika michezo mfano timu ya Serengeti Boys ambayo imekwenda mpaka AFCON U17 halikadhalika ubingwa wa Copa Coca Cola mwaka huu, na haya ni matokeo ya kazi za Maafisa Michezo katika kuibua vipaji hivi.

Aidha, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi alisistiza kuwa tasnia ya michezo ni muhimu sana katika kukuza uchumi na ni moja ya sekta inayotoa ajira nyingi kwa wanamichezo na ndiyo yenye watu wanaongozwa kulipwa fedha nyingi hivyo sekta hii ikisimamiwa vyema inaweza kulipeleka taifa mbali katika maendeleo.

[caption id="attachment_49816" align="aligncenter" width="1000"] Jonas Tiberoha akiwasilisha mada ya “Masoko,Udhamini na Maandalizi ya Maandiko katika Michezo” wakati wa kikao kazi cha Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara kilichofanyika kwa siku mbili (12 – 13,Desemba 2019) Jijini Dodoma kilichongozwa na Kauli Mbiu “Michezo kwa Afya,Ajira na Maendeleo ya Viwanda”[/caption] [caption id="attachment_49817" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara waliohudhurua Kikao Kazi cha siku mbili (12 – 13,Desemba 2019) kilichoongozwa na Kauli Mbiu “Michezo kwa Afya,Ajira na Maendeleo ya Viwanda” mara baada ya kufunga kikao hicho leo Jijini Dodoma.[/caption]

“Nimatarajio yangu kuwa kikao kazi hichi kitaleta matokeo chanya na maafisa hawa wataenda kusimamia vyema michezo katika maeneo yao na kuondoa dhana potofu ya watu kudharau michezo, pia wataibua vipaji vipya vya wanamichezo kama wanariadha mahiri zaidi ya akina Philbert Bayi,Suleiman Nyambui na Mwinga Mwanjala. Tanzania ina watu wengi sana na tuna uwezo wa kuibua vipaji vikubwa vitakavyo leta medali za dhahabu” alisema Dkt.Possi.

Pamoja na hayo Dkt.Possi alisisitiza kuwa Tanzania ina idadi kubwa ya ambao miongoni mwao wapo wengi wenye vipaji hivyo ipo haja maafisa michezo hao kuhakikisha katika maeneo yao wanafanya kazi kubwa ya kuibua vipaji haswa kwa vijana kwani hao ndiyo nguvu kazi ya taifa.

Halikadhalika Afisa Michezo kutoka Wilaya ya Siha Bibi.Neema Joseph alishukuru uongozi wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuandaa kikao kazi ambacho mbali na kuwapatia elimu ya kuandaa maandiko ya kuomba ufadhili katika michezo pia amejifunza mambo mengi ambayo alikuwa hayajui na hivi sasa wilaya yake haitaenda kuwa kama ilivyokuwa awali kutoka na mafunzo aliyopata.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi