[caption id="attachment_44930" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Augustine Mahiga akikaribishwa katika Banda la Benki ya TIB na Bw. Daud Masele (kulia) wakati wa Maonesho 43 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.[/caption]
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Waziri wa Sheria na Katiba, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ametembelea Banda la TIB ‘Group’ linalojumuisha taasisi za Benki ya Maendeleo TIB, Benki ya Biashara ya TIB ‘Corporate’ na Dawati la Huduma za Bima wakati wa Maonesho 43 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika Banda hilo alipata fursa za kujionea shughuli za uwekezaji zilizofanywa tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo mnamo mwaka 1970.
[caption id="attachment_44931" align="aligncenter" width="750"]Akizungumzia nafasi ya taasisi za kifesha katika ukuzaji wa uchumi wa nchi na kuijenga Tanzania ya Viwanda, Balozi Dkt. Mahiga alisema mabenki hasa ya maendeleo kama TIB yana nafasi kubwa katika kutekeleza mipango ya serikali ya kuimarisha uchumi wa nchi kwa kutoa mikopo ya muda mrefu yenye kuchochea maendeleo katika kukuza biashara,kuongeza ajira, kuwezesha uanzishwaji wa viwanda.
Balozi Dkt. Mahiga alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa ya uwepo wa Benki ya Maendeleo ya TIB ili kuweza kupata mikopo na misaada ya kitaalamu katika uendeshaji wa miradi yao.