Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Dkt. Kalemani Ataka Mradi wa Umeme Bonde la Mto Rufiji Kukamilika kwa Wakati
Feb 15, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_40496" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mradi wa kufua Umeme katika Bonde la Mto Rufiji ambapo aliwataka wakandarasi hao kumaliza mradi huo katika muda uliopangwa na kuwasisitiza kuanza kazi mara moja baada ya makabidhiano hayo.
[/caption] [caption id="attachment_40493" align="aligncenter" width="1000"] -Msimamizi wa Mradi wa kufua Umeme katika Bonde la Mto Rufiji Mhandisi Justus Mtolera na Muwakilishi wa Makampuni ya Arab Contractors na Elsewedy Electric Mhandisi Ahmed Ouda wakisaini nyaraka za Makabidhiano ya mradi tayari kwa Utekelezaji.[/caption]
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, RUFIJI
Serikali imetoa wito kwa Wakandarasi kutekeleza Mradi wa kufua Umeme kwa njia ya Maji mto Rufiji( RHPR)  kwa uaminifu, wakati na weledi mkubwa
Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Nishati Dkt. Merdad Kamemani wakati wa halfa ya makabidhiano ya eneo la ujenzi wa Mradi huo kwa Wakandarasi Arab Contractors- Osman A. Osman & na Elsewedy Electric kutoka Misri.
" Niwaombe wakandarasi wasitoke eneo la mradi kwani miundombinu ipo, tusingependa kugeuka nyuma, mradi huu uwe kielelezo kwa miradi mingine nchini" ameeleza Dkt. Kalemani
Aidha, Waziri Kalemani ametaja manufaa mbalimbali ya Mradi huo ikiwemo uwepo wa umeme wa uhakika na wa kutosha utakaosaidia maendeleo ya uchumi wa viwanda na wananchi kwa ujumla.
[caption id="attachment_40492" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akikata utepe katika eneo la mrafi wa umeme wa bonde la mto Rufiji kuashiria kuanza kazi ya ujenzi wa Mradi huo baada ya kuwakabidhi makampuni ya Arab Contractors na Elsewedy Electric kutoka nchini Misri, Kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu na kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.[/caption]
"Pia mradi huo utaboresha shughuli za utalii kwasababu ya ukubwa wa bwawa hilo katika ndani ya Tanzania na afrika hivyo kupelekea kuongezeka kwa pato la taifa nchini" ameongeza Dkt. Kalemani.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Arab Contractors Wael Hamdy amempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kutekeleza miradi mbalimbali katika maeneo mengi nchini.
[caption id="attachment_40494" align="aligncenter" width="1000"] Msimamizi wa Mradi wa kufua Umeme katika Bonde la Mto Rufiji Mhandisi Justus Mtolera na Muwakilishi wa Makampuni ya Arab Contractors na Elsewedy Electric Mhandisi Ahmed Ouda wakionesha nyaraka za Makabidhiano ya mradi tayari kwa Utekelezaji.[/caption]
"Mradi huu sio kwa manufaa ya Watanzania au Wamisri tuu bali kwa Waafrika nzima, hivyo nawaahidi hatutawaangusha tutafanyakazi kwa weledi na kumaliza kwa wakati" amesema Hamdy.
Nae Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango imejipanga kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati.
[caption id="attachment_40497" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mradi wa kufua Umeme katika Bonde la Mto Rufiji ambapo aliwataka watanzania kujivunia kuwa sehemu ya historia katika utekelezaji wa mradi huu.[/caption]
"Watanzania wanajisikia faraja kubwa kuwa sehemu ya uandishi wa historia sahihi kwa taifa letu kwa kutekeleza mradi huu mkubwa hivyo tumpongeze Rais Dkt.  John Magufuli kwa maono sahihi kwa watanzania" ameongeza Dkt. Kijaji.
Aidha,  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, amesema kuwa ujenzi wa mradi huo utajumuisha bwawa kuu aina ya (Rollar Compacted) lenye uwezo wa kutunza maji takribani mita za ujazo bilioni 34 na  kituo cha kufua umeme zenye uwezo wa MW 2,115.
[caption id="attachment_40498" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mradi wa kufua Umeme katika Bonde la Mto Rufiji ambapo aliahidi kuusimamia mradi huo ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati[/caption]
"Pia patajengwa majengo ya ofisi, karakana, makazi, stoo na huduma za jamii kwa ajili ya uendeshaji wa kituo," amesema Dkt. Mwinuka
Dkt. Mwinuka amesema katika utekelezaji wa mradi huo, kutakuwa na Wataalamu wa mradi kwa ajili ya kuangalia ubora wa utendaji kazi wa mkandarasi.
[caption id="attachment_40495" align="aligncenter" width="1000"] Msimamizi wa Mradi wa kufua Umeme katika Bonde la Mto Rufiji Mhandisi Justus Mtolera akitoa maelezo ya mradi kwa viongozi wa Serikali waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya mradi[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi