[caption id="attachment_44502" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akizungumza na Waandishi wa Habari masuala ua uwekezaji walipokutana nao wakati wa kongamano la kujadili masuala hayo kwa wawekezaji wa Kimarekani, kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, kushoto kwake ni Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Dkt. Inmi Patterson.[/caption]
Na.Mwandishi Wetu –MAELEZO.
Serikali imesema wawekezaji wa nje na wale wa ndani ya nchi wanapewa heshima na thamani sawa sawa na hakuna mahala popote ambapo kumekuwa na ubaguzi wa kiuwekezaji wala wa utoaji wa vibali ama urasimu wa aina yoyote ambao unawakwamisha.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia uwezeshaji Angelah Kairuki alipozungumza kwenye mjadala maalum ulioandaliwa na ubalozi wa Marekani kwa kushirikiana na chama cha wafanyabiashara wa marekani hapa nchini, uliofanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Waziri Kairuki amesema, serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli imeendelea kuboresha mazingira ya uwezeshaji kwa wawekezaji wa ndani na wale wa nje ya nchi na dhamira yake ni kuendelea kuwasaidia ili wafanya biashara na uwekezaji wao bila vikwazo vyovyote.
“Dhamira ya dhati ya Mh.Rais katika kusimamia na kuendeleza wawekezaji imejidhihirisha bayana na hivi karibuni tu aliwaalika wafanyabiashara na wawekezaji Ikulu Jijini Dar es Salaam ili kuwasikiliza na kuwasaidia kutatua kero zao” Alisema Waziri Kairuki.
[caption id="attachment_44504" align="aligncenter" width="800"]Amesema juhudi za Rais Magufuli za kuendeleza uwekezaji hazikuanza leo ndio maana akaamua kumteua yeye kama Waziri anayeshughulikia uwekezaji, hii inaonyesha namna anavyojali uwekezaji na yeye na timu yake akiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wamejipanga kuhakikisha kunakuwa na uwekezaji wenye tija.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.Palamagamba Kabudi amesema, kila mahala serikali inaendelea kuboresha miundombinu ikiwemo ya reli, barabara bandari na hata usafiri wa anga ili kurahisisha uwekezaji hapa nchini.
“Katika kulisimamia hili serikali pia imeendelea kudhibiti vitendo vya rushwa na ufisadi,lakini pia imeendelea kuondoa urasimu usio wa lazima ambao unarudisha nyuma juhudi za kukuza uwekezaji hapa nchini” Alisema Prof.Kabudi.
Aidha Prof.Kabudi amesema serikali pia imeendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwaajili ya kuiwezesha kuendelea kujenga miradi mikubwa ya kimkakati, lakini pia imeendelea kuhakikisha inawaelimisha wawekezaji kwamba juhudi za kukusanya mapato hazina lengo la kumuumiza mwekezaji na mfanyabiashara.
Naye Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini, Dkt.Inmi Patterson majadiliano hayo yamekuja wakati muafaka mabapo serikali ya Tanzania inaendeleza jitihada za kuimarisha uchumi na pia kuwawezesha wawekezaji na wafanyabiashara.