Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Watendaji Sekta ya Sera na Mipango Serikalini Wajengewa Uwezo
Nov 09, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_37979" align="aligncenter" width="858"] Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Shabani akifungua kikao cha siku moja kilichowashirikisha Wakurugenzi wa Sera na Mipango, Wakurugenzi wasaidizi, Maafisa Mipango wa Halmashauri za mkoa wa Doodma kikilenga kuwajengea uwezo katika kupanga mipango na Sera, kikao hicho kimeandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi.[/caption]

Frank Mvungi

Watendaji wa Sekta ya Sera na Mipango Serikalini wajengewa uwezo ili kuwezesha kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kusaidia katika kupunguza umasikini na kuzalisha ajira.

Akizungumza leo Jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Shabani amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuona kuwa wataalamu hao wanakuwa na uwezo  unaoendana na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayolenga kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

 “ Tunatekeleza mpango wa pili wa maendeleo na Dira ya Taifa ya 2025 inayolenga kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wetu”;

[caption id="attachment_37980" align="aligncenter" width="823"] Mtaalamu wa Sera na Mipango kutoka Taasisi ya Uongozi Dkt. Ubardus Tumaini akizungumza kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Prof. Joseph Semboja wakati wa ufunguzi wa kikao cha siku moja leo Jijini Dodoma. kikao hicho kimeandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi.[/caption]

Kikao hicho kimeandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi na kuwashirikisha wakurugenzi wa Sera na Mipango, Maafisa Mipango wa Halmashuri za Mkoa na Jiji la Dodoma.

Akifafanua amesema kuwa  wataalamu wa Sera na Mipango watawezeshwa kutekeleza  majukumu yao kwa weledi zaidi kutokana na uzoefu watakaopata kutoka kwa wataalamu waliobobea katika masuala ya Sera na Mipango wakati wa kikao hicho.

 Kwa upande wake Dkt. Ubardus Tumaini  akizungumza kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja amesema kuwa Kikao hicho cha siku moja kinalenga kuwapa ujuzi zaidi wataalamu wa Sera na Mipango ili kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Aliongeza kuwa Taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na Serikali katika maeneo ya kujenga uwezo kwa Viongozi waandamizi Serikalini, Kufanya Tafiti na kuandaa mijadala.

Sehemu ya watoa mada  katika kikao hicho wametoka nchini india na wengine kutoka hapa nchini.

[caption id="attachment_37981" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya washiriki wa kikao cha siku moja lkilichowashirikisha Wakurugenzi wa Sera na Mipango, Wakurugenzi wasaidizi, Maafisa Mipango wa Halmashauri za mkoa wa Doodma kikilenga kuwajengea uwezo katika kupanga mipango na Sera. kikao hicho kimeandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi.[/caption] [caption id="attachment_37982" align="aligncenter" width="900"] Mtaalamu wa Sera na Mipango kutoka nchini India Prof. Probhat Patrik akiwasilisha mada wakati wa kikao cha siku moja lkilichowashirikisha Wakurugenzi wa Sera na Mipango, Wakurugenzi wasaidizi, Maafisa Mipango wa Halmashauri za mkoa wa Doodma kikilenga kuwajengea uwezo katika kupanga mipango na Sera. kikao hicho kimeandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi.
                                               (Picha zote na Frank Mvungi)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi